Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya Mji wa Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa umma kuleta tija
katika utendaji kazi wao ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili, 2023 kwa mara ya kwanza
ambapo alielekeza kuwa, anataka utumishi wa umma wenye tija kwa kila
mtumishi ili kutoa huduma bora kwa mendeleo kwa Taifa.
Sehemu ya watumishi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya Mji wa Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mhe. Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa
Umma wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoani Pwani akiwa kwenye ziara
yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na changamoto
zinazowakabili watumishi wa umma mkoani humo.
“Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alieleza wazi kuwa halmashauri
zake, watendaji na watumishi wote ni lazima wawe na tija katika utekelezaji
wa majukumu yao ili kuleta maendeleo nchini,” amesema Mhe. Kikwete.
Vile vile, Mhe. Kikwete amewataka watumishi hao kubadilika ili kuendana
na matakwa ya Serikali ya Awamu ya Sita ikiwemo uaminifu katika
utekelezaji wa miradi mbambali ya maendeleo nchini na kwa kuzingatia
ubora.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon akitoa utambulisho wa viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha kabla ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili katika halmashauri hiyo.
Aidha, Mhe. Kikwete amesema kuwa, mafanikio ya taasisi au taifa lolote
yanategemea aina ya watumishi wanaoitumikia Serikali yao wakati wa
utekelezaji wa majukumu ambapo wakitekeleza kwa weledi na ufanisi
mkubwa yataleta chachu kwa maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mji Kibaha, Mhandisi Mshamu Munde
amemshukuru Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kufanya ziara katika mkoa huo
na kuahidi kuwa yeye pamoja na watumishi wenzake watatekeleza
maelekezo yote aliyoyatoa kwani kwa kutokufanya hivyo itakuwa ni utovu
wa nidhamu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa
2
Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi wa umma pamoja na kukagua
utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika mkoa huo.