•Oktoba 2023 mitambo mitano itatolewa mkoani Dodoma
- Sekta inachangia 56 % ya fedha za kigeni
Serikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya uchorongaji wa miamba kwa ajili ya utafiti wa kina wa Madini.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 25 , 2023 na Waziri wa Madini ANTONY Mavunde wakati akiongea katika kipindi cha Jambo Tanzania (TBC1) kutokea viwanja vya maonesho vya EPZ bomba mbili mkoani Geita.
Akielezea kuhusu mkakati wa VISION 2030 Madini ni Maisha na Utajiri, Mavunde amesema kuwa Serikali imejipanga kufanya utafiti wa Madini nchi nzima kwa lengo la kupata taarifa zitakazo weza kufungamanisha sekta ya Madini na Sekta nyingine za kiuchumi.
Akifafanua hali ya utafiti wa Madini amesema mpaka sasa utafiti wa kina umefanyika kwa asilimia 16 tu ambazo taarifa zake ndio zinatumika lengo la Serikali ni kuongeza taarifa kupitia tafiti nyingine ziitakazofanywa na GST.
Mpaka sasa Sekta ya Madini inachangia asilimia 56 ya Fedha za kigeni ambazo zinachangia asilimia 9.1 ya pato la Taifa(GDP) , hii ni kwa utafiti wa 16% uliofanyika , hivyo kufikia 2030 tutakuwa tumefanya utafiti nchi nzima.
Sambamba na hapo Mhe. Mavunde ameeleza kuwa Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira zitaendeleza juhudi za kutunza mazingira kama Sheria zinavyoelekeza.
Pia Waziri Mavunde ameshiriki zoezi la upandaji miti katika viwanja vya maonesho vya EPZ.
1 Comment
The area that now makes up Pakistan kept its status as one of the main cultural and political hubs of South Asia for over 300 years cheapest priligy uk Cardiogenic Pulmonary Edema The most common cause of pulmonary edema is heart disease, such as acute myocardial infarction, congestive heart failure CHF, coronary artery disease CAD, cardiomyopathy, heart valve problems, and hypertension which enlarges the heart