KITAIFA

MJEMA: VIJANA NENDENI MKAWE CHACHU YA MABADILIKO CHANYA NCHINI, KUKIPIGANIA NA KUKILINDA CCM

MJEMA: VIJANA NENDENI MKAWE CHACHU YA MABADILIKO CHANYA NCHINI,  KUKIPIGANIA NA KUKILINDA CCM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Sophia Edward Mjema Leo Tarehe 11 Juni 2023, ameshiriki kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya seneti ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam.

Mama Mjema amewasisitiza Vijana wa vyuo na vyuo vikuu kuwa chachu ya mabadiliko chanya Nchini na kuendelea kukipigania na kukilinda Chama na Viongozi wake Hususan Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan.

” Hatutokubali, Hatuko tayari kuona Mwenyekiti wetu anachezewa chezewa. Mwenyekiti wetu ni mtu imara na makini aachwe afanye kazi ya kuleta maendeleo nchini”.

Mahafali ya seneti ya mkoa wa dar es salaam , yalihudhuriwa na takribani wanafunzi 500, kutoka matawi ya vyuo 43 , Jijini Dar es salaam.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *