Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI imeanza kutoa matibabu ya kibingwa kwa Godson Mwaipopo (7) ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kambi ya Matibabu ya kibingwa yaliyokuwa yanafanyika Mkoani Arusha.

Mtoto Godson ni miongoni mwa mamia ya watoto na watu wazima waliogundulika kwenye Kambi hiyo ya Matibabu iliyokuwa ikiratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ambapo Rais Samia amejitolea kugharamia matibabu yao kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na hospitali na taasisi za afya za umma.

Joyce Mwasakapwela, mama mzazi wa Godson aliyesafiri kwenda Dar es Salaam kusimamia matibabu ya mwanae akiambatana na Mume wake Isaac Mwasakapwela kwa gharama za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na wananchi waliomchangia nauli ya kutoka mkoani Mbeya kuifuata kambi ya matibabu mkoani Arusha, amesema anaamini kuwa mtoto wake atarejea katika hali yake ya kawaida.

About Author

Bongo News

1226 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *