Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiwa katika
kikao cha kuwasilisha na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kabambe
wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa
Rais jijini Dodoma tarehe 23 Agosti, 2023.
Serikali imesema Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (2022-2032) umeweka msingi wa mipango na bajeti shirikishi ya
usimamizi wa mazingira katika ngazi zote na kuzingatia sekta mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati wa kikao cha kuwasilisha Taarifa ya
utekelezaji wa Mpango huo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na
Mazingira jijini Dodoma tarehe 23 Agosti, 2023.
Amesema kwa kutambua na kuzingatia fursa na changamoto zilizopo, Ofisi
itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje kuhakikisha
maeneo ya kipaumbele yaliyobainishwa kwenye Mpango yanatekelezwa na
kujumuishwa kwenye mipango yao ya utekelezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa
Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma tarehe 23 Agosti, 2023.
Dkt. Jafo amesema kuwa Mpango Kabambe unatekelezwa kwa kuzingatia
sekta muhimu kama Kilimo ambayo uwekezaji mkubwa umefanyika ikiwemo
uchimbaji wa malambo kwa ajili ya umwagiliaji katika maeneo yaliyoathiriwa
na ukame kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa kupanda kwa Bajeti ya Kilimo kutoka shilingi bilioni 261 hadi
zaidi ya shilingi bilioni 900 kunaakisi kazi kubwa inayofanyika mathalan
shughuli za umwagiliaji zinachangia katika upande wa mazingira.
“Leo hii tunaposema ujenzi wa malambo 114 ni almost shilingi bilioni 236, kwa
kweli tumshukuru sana Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani huo
ni uwekezaji mkubwa sana na anachozungumza kule katika mikutano ya
kimataifa ndio hiki ambacho kinaonekana sasa,“ alisema.
Tayari Wizara ya Kilimo imetoa mafunzo kuhusu kilimo kinachohimili
mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima 1,500 katika Halmashauri za Hanang,
Kongwa, Kilombero, Kahama, Babati, Makambako, Ludewa, Makete, Kyela,
Mbinga na Nyasa na maafisa ngazi ya halmashauri 30 katika za Tarime Mji,
Rorya na Serengeti.
Aidha, Dkt. Jafo alitaja sekta nyingine kama Nishati ambapo uwekezaji
mkubwa wa nishati safi ya kupikia unaendelea kufanyika ikiwemo ni sehemu
ya kupunguza matumizi ya kuni na mkaa yanayochangiwa na ukataji miti.
Hali kadhalika, alibainisha kuwa uchimbaji wa malambo kwa ajili ya
kunyweshea mifugo ni hatua mojawapo inayosaidia kupunguza vitendo vya
baadhi ya wafugaji kunyweshea mifugo yao kwenye vyanzo vya maji.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa mafunzo kwa wafugaji 184 kuhusu ufugaji
endelevu unaozingatia hifadhi ya mazingira na kuhimili mabadiliko ya
tabianchi. Vilevile, elimu imetolewa kwa wavuvi 204 Bwawa la Nyumba ya
Mungu (87) na Bwawa la Mtera (117) kuhusu kupunguza athari za uharibifu
wa mazingira unaotokana na uvuvi usiokuwa endelevu.
Alisema Uchukuzi umechangia katika utekelezaji wa Mpango Kabambe wa
Mazingira kwani mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) itakayotumia umeme badala ya
mafuta mazito utasaidia katika kupunguza hewa ya ukaa hivyo kulinda
mazingira.
“Jamii inaendelea kuhamasishwa kuthamini mazingira na kuunga mkono
juhudi mbalimbali za Serikali za kupambana na uharibifu wa mazingira ili
kuchochea ukuaji wa kiuchumi, ustawi ya jamii na Tanzania ya kijani,“
alisisitiza.
1 Comment
TPE is a great material for anybody looking to have a sex doll made.As compared to other plastics and materials,ラブドール メーカー