Uncategorized KIMATAIFA KITAIFA

MSIBWETEKE SEKTA YA UVUVI AFRIKA INATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE  KUCHANGIA PATO LA TAIFA:DKT BITEKO

MSIBWETEKE SEKTA YA UVUVI AFRIKA INATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE  KUCHANGIA PATO LA TAIFA:DKT BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wadau wa sekta ya uvuvi barani Afrika kuhakikisha wanaifanyia kazi sekta ya uvuvi ili kuhakikisha inachangia kwenye pato la Taifa kwa kuhakikisha rasilimalizi za uvuvi zinalindwa.

Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Mei 5, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wavuvi kufanyika baranı Afrika sambamba na Maadhimisho ya miaka 10 ya mafanikio ya sekta ya uvuvi wenye lengo la kutathmini sekta ya uvuvi ilipotoka, ilipo sasa na inapoelekea na kushirikisha wadau mbalimbali,taasisi zinazowasaidia wavuvi wadogo zilizoko Afrika na kwingineko duniani.

“ Nitoe wito kwenu wadau wa sekta ya uvuvi nchini kuhakikisha mnawapa kipaumbele wavuvi wadogo kwani ndio wanaochangia takribani asilimia 95 ya uvuvi wote Tanzania”, amesema Dkt.Biteko

Ameongeza “Takwimu zinaonesha kuwa nchi Tanzania inazalisha wastani wa tanı 475,579 za samaki katı ya hızo tani 429,168 zinatokana na uvuvi katika maji ya asılı na kuchangia kiasi cha shilingi trilioni 3.4 ambapo ni karibu na asilimia1.9 kwa mwaka”.

Aidha, Dkt. Biteko amesema licha ya jitihada zinazochukuliwa kwenye sekta ya uvuvi Tanzania Kama ilivyo kwa bara la Afrika bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi,ushirikishwaji mdogo wa wadau katika usimamizi wa shughuli za uvuvi hususani wanawake na vijana pamoja na upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa ni heshima kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa kwanza Afrika wa Wavuvi Wadogo ambao chimbulo lake ni Mkutano wa kuadhimisha Mwaka wa Kimataifa wa Wavuvi Wadogo na Wafugaji Viumbe kwenye Maji (IYAFA) uliofanyika Rome nchini Italia Machi, 2023.

Ameongeza kuwq lengo la Mkutano huo wa Kwanza wa Wavuvi Wadogo Afrika ni kutoa fursa kwa Wavuvi Wadogo kushiriki na kupaza sauti zao juu ya kuboresha uvuvi mdogo ikiwa ni pamoja na kuwezesha ushirikishwaji wa wavuvi wadogo kwenye michakato ya uundwaji na utekelezaji wa sera, sheria, kanuni, mipango na mikakati yote inayohusu wavuvi wadogo.  
 
“Ni muhimu kusema kwamba uchaguzi wa Tanzania haukuwa kwa bahati, ila ni kwa kutambua umuhimu wa uvuvi mdogo kwenye nchi yetu, na hatua ambazo nchi imechukua katika kuandaa na kutekeleza Mpango wa Nchi wa Utekelezaji wa Mwongozo wa Hiyari wa Uvuvi Mdogo”, amesema Ulega.

Amefafanua kuwa Kauli mbiu ya Mkutano huo “Muongo mmoja wa Maendeleo: Kuongelea baadaye ya Uvuvi Mdogo Endelevu “ ilichaguliwa kutokana na kusherekea miaka kumi ya utekelezaji wa Mwongozo wa Hiyari wa  Uvuvi Mdogo ili kufikia uvuvi mdogo endelevu. Mkutano huu utafanya tathmini ya hali halisi ya utekelezaji Mwongozo huo wa hiyari, sambamba na utekelezaji wa muundo wa kisera na Mkakati wa Mageuzi ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Afrika.

“Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza Duniani kuandaa Mpango kazi wa kutekeleza Mwongozo wa Hiyari wa wavuvi wadogo ambapo katika mkutano huu tutapata fursa ya kueleza uzoefu wetu kwa nchi nyingine.” Amesisitiza Mhe. Ulega.
 
Waziri wa Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi kutoka nchini Malawi,  Dkt. Michael Bizwick Usi amesema kuwa kupitia mkutano huo nchi wanachama wanapaswa kujadili masuala yanayohusu sekta ya uvuvi mdogo barani Afrika na kuangalia namna bora ya kuboresha kutokana na changamoto zilizopo.

Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Ang’ele Makombo N’tumba amesema kuwa kuna haja ya kuwasaidia wanawake katika sekta ya wavuvi wadogo na kuwa SADC kwa kushirikiana na wadau watasaidia nchi wanachama ili kuboresha sekta hiyo pamoja na kuzuia uvuvi haramu.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), Dkt. Tipo Nyabenyi Tito amesema licha ya kuwepo kwa changamoto zinazowakabili wavuvi wadogo ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na kuwa FAO itashirikiana na wadau wa sekta ya wavuvi wadogo kwa kukuza uelewa na uwezo kwa wavuvi hao.

Kwa upande wake, Rais wa Mtandao wa Wavuvi Wadogo Barani Afrika,  Gaoussou Gueye amesema kuwa sekta ya uvuvi mdogo ni muhimu hivyo inatakiwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuongeza tija ya shughuli za uvuvi na kuwa wanawake wako katika sekta mbalimbali kuanzia ukusanyaji wa samaki hadi kuuza kwa walaji.

“Kama tunataka kusaidia uvuvi uwe endelevu lazima tuwe na mazingira wezeshe kwa wanawake ili kuleta usalama wa chakula katika bara la Afrika na utoshelevu wa chakula, katika uchumi wa buluu tunapaswa kulinda uchumi wetu kwa kukuza sekta kwa maendeleo ya Afrika.” Amesema Gueye.

About Author

Bongo News

12 Comments

    SoundCloud to MP3 is a game-changer for me. I can save all my favorite tracks and listen offline.

    The emerging hip-hop talent on SoundCloud is incredible.

    Откройте путь к улучшенной версии себя – перейдите
    по ссылке на :~:text=%D0%A2%D1%80%D0%B8%20%D0%B4%D0%BE%D0%B3%D0%BC%D0%B0%D1%82%D0%B0-

    Приветствуем в увлекательную вселенную кинематографа отличного качества онлайн – топовый онлайн
    кинотеатр. Смотреть фильмы в интернете правильный выбор в 2024 году.
    Киноленты онлайн высочайшем качестве sizok.ru

    Cells were treated with 20 nM everolimus or vehicle every 48 h for 17 days priligy amazon colospa minoxidil finasteride combination results The union already says that eight out of LabourГў s 13 strong contingent in the European parliament are Гў Unite MEPsГў

    Excellent post. I was checking continuously this blog and I’m impressed! Very helpful info particularly the last part 🙂 I care for such info a lot. I was looking for this particular information for a very long time. Thank you and good luck.

    such as rubber toys,balls,ラブドール 画像

    On the ground, the adult two legged torasemide o lasix flying dragon let out a mournful whistle and fell to the ground better business bureau online pharmacy priligy

    Talk with your healthcare provider if you re taking blood thinners such as warfarin Coumadin, Jantoven [url=https://fastpriligy.top/]priligy premature ejaculation pills[/url]

    can you buy cytotec pills The Texas Supreme Court concluded that the student- athlete did not have a fundamental right to participate in extracurricular activities

    nogensinde løbe ind i problemer med plagorisme eller krænkelse af ophavsretten? Mit websted har en masse unikt indhold, jeg har

    Dead written content, Really enjoyed studying.

    Great website. Plenty of helpful information here. I am sending it to some friends ans also sharing in delicious. And naturally, thank you in your sweat!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *