KITAIFA

MSIGWA: SERIKALI YA AWAMU YA SITA INA NIA NJEMA NA BANDARI ZETU

MSIGWA: SERIKALI YA AWAMU YA SITA INA NIA NJEMA NA BANDARI ZETU

Sakata la ubinafsishaji wa Bandari ya Dar es Salaam limeendelea kutolewa ufafanuzi na Serikali kwa kuwatoa hofu Watanzania kwamba wasiwe na shaka kwani kila kitu kitakwenda sawa kwani utaangalia maslahi mapana ya nchi tofauti na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa ambao wanadaiwa kupotosha jamii kwamba mkataba huo umeshasainiwa.
Akizungumza na Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) Dar es Salaam leo Juni 9, Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.
Sema kuwa siku mbili tatu zilizopita kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya dhamira ya Serikali ya uendelezaji na uendeshaji wa bandari, kukaribisha uwekezaji kwenye maeneo hayo ya bandari.
“Kilichojitokeza ni kwamba, mwaka jana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikutana na mtawala wa Dubai wakazungumza, baada ya hapo nchi zetu zikaingia makubaliano ya kushirikiana katika uendelezaji na uendeshaji wa maeneo ya bandari. Baada ya makubaliano hayo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ndogo ya 33 baada ya makubaliano hayo yanatakiwa yakaridhiwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hivyo Serikali imewasilisha mkataba ule kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili lifanye mchakato wake na kuridhia.
“Bunge nao wametangaza kulingana na mchakato wao kupokea maoni ya wadau, baada ya hapo watachakata, watatoa mchango wao kwa Serikali kuhusiana na mkataba huo. Kwa hivyo maneno yaliyoenea siku mbili tatu hizi kwamba bandari yetu imeuzwa, mara mkataba hauna mwisho, BANDARI YA DAR ES SALAAM HAIJAUZWA, kilichoingiwa ni mkataba wa kukubaliana kushirikiana, yaani ile tu dhamira ya kwamba Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai zipo tayari kwenye kushirikiana kuendeleza bandari, baada ya makubaliano hayo ambayo tunatakiwa tuwe tumeyakamilisha ndani ya miezi 12, tusipokamilisha ndani ya muda huo mkataba huu unaondoka, tukikamilisha baada ya hapo tunakwenda kwenye mikataba ya utekelezaji, ndio tutapokwenda kusema bandari yetu tutakodisha, tutapangisha, tutawapatia kwa muda fulani au tutawaajiri tukawapa kazi fulani za kufanya, hiyo itakuja baadaye, ndiyo itakuja na muda maalumu wa kutekeleza mikataba ambayo tutaingia, ambayo mpaka sasa bado.
“Wengi wanasema kuna MOU kati ya kampuni ya DP World ya Dubai na TPA. MOU nayo ni ya kusema kwamba tuko tayari kushirikiana, kwasababu Serikali imefanya mawasiliano na waendeshaji wakubwa wa bandari duniani na wote tumewapima. Hawa DP World tumewaona, siyo kwamba tumewekeana mkataba, tumeona ndio tunaweza tukapata manufaa zaidi tukishirikiana nao kuliko wengine. Nakumbusha tena, bado hatujasainiana nao mkataba, yale ni makubaliano tu yakushirikiana, baada ya hapo tutasainiana nao mikataba ya utekelezaji endapo tutafikia hatua hiyo.
Tunafanya hivyo kwa sababu haina ubishi, bandari yetu ya Dar es Salaam na nyingine zote Tanzania ufanisi upo chini sana. Wataalamu wanasema, kwa mfano Bandari ya Dar es Salaam ambayo ndio kubwa sasa hivi inapitisha mzigo chini ya tani milioni 20 kwa mwaka, wakati ina fulsa kubwa ya kuhudumia nchi zaidi ya nane zisizokuwa na bahari ambazo zinaizunguka Tanzania. Wataalamu wetu wanatuambia tukifanya uwekezaji mzuri, tukaweka utaalamu wa kutosha uendeshaji wa bandari, tukaweka teknolojia za kisasa za ushushaji na upakiaji mizigo tunaweza kuhudumia zaidi ya tani milioni 58 kwa mwaka na kupata mapato zaidi.
“Uwekezaji kwenye bandari siyo mchezo, hivi ninavyozungumza na nyinyi kuna uwekezaji mkubwa tumeufanya, miaka mitatu, minne iliyopita, tumekopa ela ambazo tutakuja kuzilipa, tumejenga gati Ro-Ro linaloshusha magari pale bandarini, tumeongeza kina gati namba 1-7 ili ziweze kupokea meli kubwa, tutakwenda kuongeza kina kwa gati namba 8-11 na tunapanua ile njia ya kuingia meli, tumetumia fedha tulizokopa zaidi ya trilioni 1.2 kwa ajili ya kazi hii, hapo tumejenga gati moja tu. Wataalamu wanatuambia, ili tuweze kupata manufaa kwenye bandari yetu lazima tujenge gati mpya tisa, sasa kama gati moja tumetumia trilioni moja na kitu, hivi hizo tisa itakuwa shilingi ngapi?
“Wanatuambia uwekezaji wa kupitisha tani milioni 58 kwa mwaka tunahitaji kutumia siyo chini ya trioni 4 kwa ajili ya kuwekeza kwenye bandari, fedha hizo hizo ndiyo tunazitumia kwenye ujenzi wa barabara, kuwapatia Watanzania maji, kuwapelekea umeme ambapo leo tunazungumza vijiji zaidi ya elfu 36, havina umeme, tuna vitongoji zaidi ya elfu 36 havina umeme, hapo tunataka kukamilisha vijiji kwanza mpaka kufikia Desemba mwaka huu, mbali na umeme tunahitaji kuwapelekea dawa, hospitali nyingi, vituo vya afya, zahanati vinahitaji dawa. Tukichukua hizo pesa zote tukaenda kuziweka kwenye bandari hizi huduma nyingine serikali itashindwa kutoa.
Aidha Msigwa aliesendelea kusema kuwa kuwa, “Duniani kote hivi sasa bandari zinaendeshwa kibiashara, zinaendeshwa na wawekezaji. Muelekeo wa Serikali ni kwamba, tunataka kuwahusisha wawekezaji katika uendeshaji wa bandari zetu, tutawakaribisha waje wawekeze ili sisi tupate mapato zaidi. Naka niwaambie ndugu zangu Watanzania bandari ya Dar es Salaam kwa mfano mwaka 2021/2022 tumezalisha shilingi trioni 1.058 ndiyo mapato ya bandari, lakini zaidi ya bilioni 600 katika hizo ni matumizi, fedha iliyobaki kama bilioni 120, kwa libandari lote hili? Bandari ni mahali tunaweza kupata pesa, tunaweza kupata mapato zaidi ya mara mia mbili ya haya endapo tutawatumia wawekezaji. Pesa tunazotumia zaidi ya bilioni 600 wataweka wawekezaji, sisi tutakwenda kuchukua mapato.
“Hatutatumia pesa za taifa zinazokwenda kuhudumia maji Watanzania wala umeme, barabara na vitu vingine, lazima tukumbushane kuwa, tumekopa ile trioni 1.2 kwa ajili ya kazi inayoendelea ya upanuzi wa bandari fedha hiyo inakwenda kuongeza deni la taifa, tukienda kukopa tena tutazidi kuongeza deni kwa taifa.
“Vilevile tutakapoifanya mikataba ya utekelezaji, serikali itazingatia maslahi ya Watanzani, tutahakikisha tunaingia mikataba yenye maslahi na Watanzania, hayo mengine yanayosemwa tumeshaingia mkataba ni upotoshaji, hakuna kitu cha namna hiyo, bali ni makubaliano ya mashirikiano. Itapokuja mikataba itakuwa ni ‘win win’, wao wapate na sisi tupate. Hatuwezi tukaa hivi, tuna bandari pale hatupati pesa zozote. Leo hii bandari yetu wastani wa meli kusubiri ni siku 9, bandari za wenzetu wameshatoka huko, sasa hivi meli ikifika inashusha mizigo hapo hapo, sisi tutasubiri mpaka lini, kila siku kuna meli 20 zinasubiri kushusha. Wenye meli hasa Uingereza hawapendi kuleta Tanzania kwasababu zinasubiri sana na mwenye meli akisubiri sana anaongeza gharama za usafirishaji, mwisho wa siku unakuja kulipa Mtanzania kwenye bidhaa zinazokuja kuuzwa, kama shati ulitakiwa uuziwe shilingi elfu 5 utauziwa elfu 7 kwasababau meli ilikaa sana baharini inasubiri.
“Kikubwa zaidi tunatafuta wawekezaji waongeze uwezo wa bandari zetu kuhifahi hata mizigo ya nafaka. Leo bandari yetu inaweza kuhifadhi nafaka tani elfu 30, haiwezi kuhifdhi zaidi ya hapo, matarajio yetu tupate uwekezaji ukataotuwezesha kuhifadhi hadi tani milioni 30, tukifika hapo tutapunguza gharama. Sasa hivi tunakwenda kufanya mapinduzi kwenye kilimo, tunataka ifikapo 2030 kikue kwa wastani wa asilimia 10, sasa hivi tuko chini ya asilimia 4. Tukienda kwenye asilimia 10 uzalishaji wa mazao ya kilimo utaongeka mara dufu, ukiongezeka tutahitaji kuyasafirisha kwenda nje ya nchi, utayasafirisha kwa bandari ipi kama yetu hapo ilipo tu inaelemewa. Lakini pia tunatekeza mradi mkubwa wa zaidi ya trioni 23 wa ujenzi wa reli, kilometa elfu moja na kiti kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, kilometa elfu tano na kitu kutoka Tabora mpaka Kigoma, reli ya kisasa (SGR), ile treni itakuwa na uwezo wa kufunga treni ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani zaidi ya elfu 10 kwa wakati mmoja. Ukishafunga treni kama hiyo, bandari uwezi ndio ule, treni itakuwa inasubiri, itakuwa ni kituko zaidi kwababu tutakuwa na treni zinasubiri na meli zinasubiri mzigo ushushwe, ndio maana tunataka kutoka huko, tunatafuta uwekezaji ambao utaongeza ufanisi kwenye bandari yetu, tunataka ikachangie mapato zaidi ya asilimia 50, tukapojumlisha na mapato mengine tutatekeleza miradi yetu mingi na tutalipa deni la taifa vizuri na mambo yetu kama nchi yatakuwa mazuri. Haya maneno mengine ni porojo za kutaka kutuondoa kwenye reli, tunakwenda kuingia mikataba ambayo inaangalia maslahi ya nchi,” alisema Msigwa.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *