Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kulia) akielekea kwenye ukumbi wa mikutano Mkoa wa Pwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuzungumza na watumishi wa halmashauri hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao. Katikati ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Maafisa Utumishi nchini kufanya
kazi kwa bidii na ubunifu ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi
kwa maendeleo ya taifa.
Mhe. Kikwete amesema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa
Umma Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na changamoto
zinazowakabili watumishi wa umma mkoani humo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
“Nataka kusikia kila Afisa Utumishi anajiwekea ratiba ya kuzungumza na
watumishi anaowasimamia ili kusikiliza maoni, malalamiko au changamoto
zozote wanazokutana nazo kwa lengo la kuboresha utumishi wa umma
nchini utakaoweza kuwahudumia wananchi kikamilifu,” amesema Mhe.
Kikwete.
Aidha, Mhe. Kikwete amewataka Maafisa Utumishi kuweka utaratibu wa
kujua mahitaji ya watumishi kwa kuzingatia hali halisi ili kukidhi haja
mbalimbali za watumishi bila kuwa na malalamiko.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mhe. Kikwete amesema kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
anataka Maafisa Utumishi hao kuwa wasemaji wa watumishi
wanaowasimamia na kutatua kero na changamoto zao.
Mhe. Kikwete amewasihi watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa
juhudi, werevu na weledi mkubwa katika kuwatumikia wananchi
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kisarawe, Bw. Baptista Kihanza ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha
kupata rasilimaliwatu ambayo imesaidia kupunguza tataizo la uhaba wa
watumishi katika halmashauri hiyo.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete anaendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa
wa Pwani ikiwa leo ni siku ya tatu akilenga kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa
umma pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika mkoa
huo ambapo leo alikuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
1 Comment
Профессиональные seo https://seo-optimizaciya-kazan.ru услуги для максимизации онлайн-видимости вашего бизнеса. Наши эксперты проведут глубокий анализ сайта, оптимизируют контент и структуру, улучшат технические аспекты и разработают индивидуальные стратегии продвижения.