Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka viongozi kote nchini kuweka maslahi ya wananchi mbele na kuacha migogoro inayotokana na ubinafsi wao.

“Hawa Watanzania hawataki migogoro yetu sisi viongozi na wakati mwingine migogoro tuliyonayo ni migogoro ya maslahi binafsi. Tumeacha kuwahudumia wananchi tunashughulikiana, tunataka huyu akwame, huyu afanikiwe kwa sababu tuna cartel (makundi),” amesema Dkt. Biteko
Akizungumza Aprili 24, 2025 Mundarara, Wilayani Longido, Dkt. Biteko amesema kuwa amani ndiyo msingi wa utoaji huduma bora “Tunataka watu waungane, wafanye kazi ya pamoja. Hakuna kitu kinachotia aibu kama unakuta kiongozi umepewa nafasi mahali fulani ama wewe una cheo mahali fulani badala ya kuzungumza shida za watu unawazungumza watu, Huyu kwako mbaya, yule mbaya, huyu mbaya, Wewe ukiulizwa uzuri wako huna cha kuonesha.”

Amesisitiza kuwa viongozi waliopata nafasi wanapaswa kumtumia mwananchi kama mteja wao wa kwanza, wa pili, na wa tatu “Viongozi tuliopata nafasi mteja wetu wa kwanza awe mwananchi, mteja wetu wa pili awe mwananchi, mteja wetu wa tatu awe mwananchi. Hawa wananchi ndiyo wanatupa uhalali wa sisi kuitwa viongozi, tukumbuke ni kwa kodi zao tupo hapa, Tusihubiri chuki. ”amesisitiza Dkt. Biteko @biteko @onwm_tanzania
6 Comments
Thanks for the auspicious writeup. It in truth used to
be a amusement account it. Look advanced to
more delivered agreeable from you! By the way, how could we communicate?
http://maps.google.be/url?q=https://t.me/Top_Spisok_Game/161
Hi there i am kavin, its my first time to commenting anyplace, when i read this piece
of writing i thought i could also make comment due to this brilliant paragraph.
Hi to all, hoow is all, I think every one is
gettying morfe ffom this website, annd yolur
visws arre fasttidious ffor neww users.
Link gacor scatter hitam : Menang Besar dengan Slot Gacor dan Scatter Hitam
Situs Togel Terpercaya dan Permainan Slot Gacor di situs sigmaslot