Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa viongozi wa Manispaa ya Ubungo, wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kwembe ya wasichana inayojengwa katika Manispaa ya Ubungo kupitia mradi wa SEQUIP.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Deogratius Ndejembi amemuagiza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI
kuunda timu maalum ya kukagua matumizi ya fedha kwenye ujenzi wa
shule ya Sekondari ya Kwembe ya wasichana inayojengwa katika
Manispaa ya Ubungo kupitia mradi wa SEQUIP.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na baadhi ya walimu na watumishi Shule ya Sekondari Kwembe, alipowasili kukagua ujenzi wa shule hiyo ya wasichana inayojengwa katika Manispaa Ubungo kupitia mradi wa SEQUIP.
Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo akiwa katika Manispaa ya Ubungo
mara baada ya kutoridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika
Sekondari hiyo ya Kwembe, licha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
kutoa fedha nyingi ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo maalum ya
wasichana ya sayansi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akielekea kukagua moja ya jengo katika shule ya Sekondari ya Kwembe ya wasichana inayojengwa katika Manispaa ya Ubungo kupitia mradi wa SEQUIP. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba.
Mhe. Ndejembi amesema, hajaridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa
ikizingatiwa kuwa awali Serikali kuu ilitoa bilioni 3 na kuongeza bilioni 1.1
na Manispaa ya Ubungo ikaongeza tena bilioni 1.2 ili kukamilisha ujenzi wa
miundombinu katika shule hiyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisikiliza kwa makini taarifa ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kwembe wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa shule hiyo ya wasichana inayojengwa katika Manispaa ya Ubungo kupitia mradi wa SEQUIP. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba.
“Nilichokiona hapa ni dalili za matumizi mabaya ya fedha iliyotolewa na
Rais Samia Suluhu Hassan, hivyo ofisi ya Rais-TAMISEMI haiko tayari
kuona fedha ikichezewa na ndio maana nimeelekeza uchunguzi ufanyike,”
Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Aidha, Mhe. Ndejembi ameutaka uongozi wa Manispaa ya Ubungo
kuongeza usimamizi na kumtaka mkandarasi kuongeza idadi ya mafundi ili
shule hiyo ikamilike na kuwapokea wanafunzi zaidi ya 200 waliopangiwa
kuripoti katika shule hiyo.

Muonekano wa moja ya jengo linaloendelea kujengwa katika shule ya Sekondari ya Kwembe ya wasichana kupitia mradi wa SEQUIP.
Akizungumzia kusuasua kwa ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya
elimu mkoani Dar es Salaam, Mhe. Ndejembi amesema wataalam na
wakandarasi wameikwamisha Serikali kutekeleza lengo la kuboresha
miundombinu kwa wakati hivyo amewataka kubadilika kiutendaji ili wawe
na tija katika maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba
ameahidi kuwa atahakikisha anawasimamia wakandarasi na mafundi
kufanya kazi usiku na mchana ili shule hiyo ikamilike na kupokea
wanafunzi waliopangiwa kuripoti katika shule hiyo.
2 Comments
The realism of the doll is astounding,ラブドール エロwith lifelike skin texture and intricately detailed facial features that make it look incredibly authentic.
История развития рулевого управления кораблем https://e-pochemuchka.ru/istoriya-razvitiya-rulevogo-upravleniya-korablem/