Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewaambia wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa nafasi na Cheo chake na nguvu zake zote amezielekeza kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha wanaojihisi kusahaulika na kutotendewa haki na watumishi wasiokuwa waaminifu na wananchi wenye fedha.
Mhe. Mkuu wa Mkoa Paul Christian Makonda ametoa kauli hiyo leo Mei 09, 2024 Ofisini kwake Mjini Arusha, ikiwa ni siku ya pili ya Kliniki yake maalum ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi akisema kuwa amefarijika kwa matumaini na wingi wa wananchi waliojitokeza ofisini kwake licha ya mvua kubwa kunyesha tangu majira ya asubuhi.
Akizungumza na Mamia ya wananchi kwenye Viwanja vya Makao makuu ya Mkoa, Mhe. Makonda ameahidi kutunza na kutekeleza kikamilifu tamanio la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kukataa dhulma na kuminywa kwa haki za wananchi hasa wananchi walio wanyonge.
Mkuu wa mkoa pia amewataka watendaji na watumishi wa ofisi yake wanaosikiliza wananchi pamoja na Mawakili wanaotoa msaada wa kisheria kwa wananchi kuongeza kasi katika kuhudumia wananchi ili kuhakikisha wananchi wote wanasikilizwa na kutatuliwa changamoto walizonazo.
Katika Hatua nyingine Mhe. Mkuu wa mkoa Paul Christian Makonda ameonesha kushangazwa na wanamitandao wanaokosoa Kliniki yake ya kuwasikiliza wananchi na kuwaambia kuwa nafasi yake siku zote ataitumia kwaajili ya kuhakikisha wananchi wananufaika kuaminika kwake na mteule wake ambaye ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyemuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
5 Comments
Those are yours alright! . We at least need to get these people stealing images to start blogging! They probably just did a image search and grabbed them. They look good though!
Regards for this grand post, I am glad I noticed this web site on yahoo.
priligy generika dapoxetine 60mg Most patients stop wearing a compression garment compression stockings or Unna boots because it feels uncomfortable
The two system sites Catholic Health Initiatives and Ascension Health each selected one or two lead sites to facilitate implementation of the NCCCP within their systems priligy prescription This complicated sorting generates a high likelihood of random apparent associations that may not be reproducible
can i order generic cytotec without prescription Although some infants recover from BPD, others have long term health problems as a result and many require intensive medical care