Kituo cha Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimetoa mafunzo ya uibuaji wa miradi inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Manispaa ya Geita.

Mafunzo hayo, yaliyotolewa na wakufunzi Dr. Abiud Bongole na Christine Kaigarula yakilenga
Kuelewa dhana ya PPP, Kuibua miradi yenye sifa za kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP, Kuandaa maandiko dhana (Project Concept Notes), Kuandaa matangazo ya miradi kwa wawekezaji
Kutumia teknolojia ya GIS katika uwekaji wa miradi kwenye ramani za Halmashauri

Katika ziara hiyo, timu ya PPPC ilikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Gombati, ambaye alisisitiza fursa zilizopo katika sekta za madini, uvuvi, viwanda, utalii wa madini na mazingira.

Pia, PPPC ilikutana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Bw. Yefred Myenzi, ambaye alielezea dhamira ya Manispaa yake katika kubaini miradi yenye tija kwa maendeleo ya mkoa.

PPPC inaendelea kutoa mafunzo katika mikoa 13 nchini kwa ajili ya kusaidia uibuaji wa miradi ya PPP kwa maendeleo jumuishi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *