Raia wa China, Xie Xiaomao, amehukumiwa kulipa faini ya Sh 2milioni au kwenda jela miaka mitano baada ya kupatikanana hatia ya kufanya biashara kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na leseni ya Benk Kuu.

Mshtakiwa huyo amehukumiwa adhabu hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukiri shtaka hilo.

Pia, mahakama hiyo , imetaifisha kiasi cha zaidi ya Sh 185milioni ambazo alikutwa nazo mshtakiwa katika sehemu yakubadilishia fedha, kuwa mali ya Serikali.

Hukumu hiyo ilitolewa Hakimu Mkazi Mkuu, Rahim Mushi, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshatakiwa kusomewa shtaka lake.

Hakimu Mushi alisema mshtakiwa amekiri shtala kale mwenyewe hivyo, mahakama hiyo ina mhukumu kulipa faini ya Sh 2milioni na akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Christine Joas, uliomba mahakama itoa adhabu kwa mujibu wa sheria.

Pia uliomba fedha alizokamatwa nazo mshtakiwa ambazo ni dola za kimarekani 64,255 pamoja na Tsh 16,797,000 zitaifishwe na kuwa mali ya serikali.

Fedha hizo ni sawa na jumla ya Sh 185,787,650

Kwa upande wake wakili wa mshtakiwa, Mrisho Abdulhakim aliomba mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwa kuwa ni mkosaji kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, raia huyo wa china anadaiwa kutenda kosa kale eneo la Supermarket ya Peninsula iliyopo Oysterbay, kati ya Januari , mwaka 2024 hadi Mei 16 mwaka 2024

Mshtaliwa anadaiwa kukutwa akifanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na leseni ya benki Kuu ya Tanzania, kinyume cha sheria.

About Author

Bongo News

23 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *