Mshtakiwa huyo ambaye mkazi wa Gongolamboto, amefikishwa Mahakamani hapo Jana naalisomewa shtaka lake na wakili wa Serikali, Eric Davis, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga.
Akimsomea hati ya mashtaka, wakili Davis , alidai kuwa mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa lake, Agost 31, 2019 eneo Ubungo wilaya ya Ilala.
Siku hiyo ya tukio, mshtakiwa anadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye e uzito wa kilo 4.14, kinyume cha sheria..
Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake, upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wapo katika hatua za kuwasilisha taarifa muhimu Mahakama Kuu, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Ruboroga baada ya kusikiliza maelezo hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 20, 2023 itakapotajwa.
Mshtakiwa alirudishwa rumande kwa sababu shtaka linalowakabili haina dhamana kwa mujibu wa sheria.