Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 100 ya Sheikh Alhabyb Omar Qullatayni Bin Muhammad Annadhiyriy iliyofanyika leo tarehe 26 Septemba 2023 Msikiti wa Ijumaa Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Masheikh kutoka nchi mbalimbali wameshiriki katika maadhimisho hayo ikiwemo Comoro, Somalia, Yemen, Kenya, Umoja wa Falme za Kiarabu na Tanzania Bara.
Vilevile maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Dini.
🗓️26 Septemba 2023
📍Msikiti wa Ijumaa Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi.