KITAIFA

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO MIUNDOMBINU YA WIZARA, AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO MIUNDOMBINU YA WIZARA, AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI

Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na
uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais, hivyo Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko
madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:

  1. Ameunda Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ambapo amemteua Prof. Kitila
    Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na
    Uwekezaji. Mhe. Prof. Mkumbo ni mbunge wa jimbo la Ubungo.
  2. Ameunda Wizara ya Fedha ambapo amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
    Nchemba kuwa Waziri wa Fedha. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Nchemba
    alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
  3. Ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo amemteua Mhe. Dkt.
    Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa wizara hiyo. Kabla ya uteuzi huu
    Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
  4. Amemteua Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume
    ya Mipango ya Taifa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mafuru alikuwa Naibu Katibu
    Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).
  5. Amemteua Bw. Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
    Fedha (Usimamizi wa Uchumi). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mwandumbya
    alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na
    Mipango.
About Author

Bongo News

5 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *