Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya
mabadiliko madogo ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, uteuzi wa Mkuu wa Mkoa,
uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na uteuzi wa Mkuu wa Wilaya kama ifuatavyo:
- Amemteua Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Mhe.
Mtanda ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora. Anachukua nafasi ya
Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee. Meja Jenerali Mzee atapangiwa
majukumu mengine. - Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Manyara. Mhe. Sendiga ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anachukua nafasi ya
Mhe. Nyerere ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa. - Mhe. Charles Makongoro Nyerere amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa. Mhe. Nyerere ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya
Mhe. Sendiga ambaye amehamishiwa mkoa wa Manyara. - Amemteua Bw. Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.
Anachukua nafasi ya Mhe. Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Mara.
Mabadiliko, uhamisho na uteuzi huu unaanza mara moja.
Uapisho wa Mkuu wa Mkoa mpya utafanyika tarehe 24 Mei, 2023 saa 10:00 jioni,
Ikulu Chamwino.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
1 Comment
What i do not realize is actually how you are no longer actually much more well-favored than you might be now. You’re very intelligent. You realize thus considerably on the subject of this subject, produced me in my opinion consider it from a lot of various angles. Its like men and women aren’t involved until it?¦s something to do with Lady gaga! Your individual stuffs outstanding. At all times deal with it up!