KITAIFA

RAIS SAMIA AFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI (SAFINA HOUSE) LA KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA, DAYOSISI YA CENTRAL TANGANYIKA, DODOMA

RAIS SAMIA AFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI (SAFINA HOUSE) LA KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA, DAYOSISI YA CENTRAL TANGANYIKA, DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na
Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Dkt. Maimbo Mndolwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma. Kushoto ni Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani kuashiria ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023. Engine katika picha ni Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Dkt. Maimbo Mndolwa pamoja na Maaskofu wengine wa Kanisa hilo nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi
ya Kitabu (Itifaki ya Biblia) kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Kanisa la Anglikana Tanzania wakiwa
kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani wakati
wakiwa kwenye eneo lenye michoro ya jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akicheza pamoja
na waimbaji wa Kwaya ya Safina wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo lililopo katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Kanisa la Anglikana Tanzania mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini
Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Muonekano wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika ambalo limefunguliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu tarehe 15 Agosti, 2023.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *