Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Februari 25, 2025 amefungua rasmi shule ya sekondari ya Wasichana Tanga.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Tanga ni taasisi ya elimu iliyojengwa wilayani Kilindi, mkoani Tanga.

Mradi huo ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita zenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wasichana, ili kuwawezesha kupata elimu bora katika mazingira salama na yenye miundombinu ya kisasa.

Mradi huu umetekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 147,000, likiwa na miundombinu ifuatayo: mabweni 12 kwa ajili ya wanafunzi.

Shule hiyo ina jumla ya vyumba vya madarasa jumla ya 12, vikihudumia wanafunzi kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne.

Pia shule ina maabara za Jiografia, Fizikia, Kemia, na Baiolojia ili kuwezesha wanafunzi kupata elimu ya vitendo katika masomo ya sayansi.

Pia kuna zahanati kwa ajili ya huduma za afya kwa wanafunzi na walimu, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na uongozi wa shule, bwalo la chakula kwa ajili ya mahitaji ya lishe ya wanafunzi wa bweni, pamoja na assembly point (eneo la mikusanyiko ya wanafunzi) kwa shughuli mbalimbali za shule.

Kwa upande wa makazi, shule ina nyumba za walimu ili kuhakikisha walimu wanapata makazi bora karibu na shule.

Pia kuna power house kwa ajili ya kupokelea na kusambaza umeme katika shule, pamoja na uwanja wa michezo kwa ajili ya shughuli za michezo na maendeleo ya vipaji vya wanafunzi.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Tanga inatarajiwa kuwa kitovu cha elimu bora, ikiwezesha wasichana kupata fursa za elimu katika mazingira mazuri na yenye vifaa vya kisasa.

About Author

Bongo News

2 Comments

    izu2ad

    Nice weblog here! Also your site a lot up very fast! What host are you the use of? Can I am getting your associate hyperlink in your host? I want my site loaded up as fast as yours lol

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *