Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisikiliza maelezo ya mnufaika wa Mpango wa kuwawezesha Vijana kwenye Mifugo (BBT life Mifugo) Rest Mgonja kuhusiana na Mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo wa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Bw. Ahmed Salim kuhusu chakula cha Mifugo wakati alipotembelea Banda la Kampuni hiyo wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Mhandisi wa Mtaani (Street Engineer) Adam Zacharia Kinyekile kutoka Tunduma Mkoani Songwe jinsi alivyobuni na kutengeneza mashine hiyo ya kuvuta maji, kupukuchua mahindi kusaga nafaka pamoja na kubeba Mizigo wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane ambapo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu kuhusu Tume hiyo inavyowasaidia wakulima wenye ubunifu mbalimbali katika
Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika kwenye viwanja vya John
Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Mwanzilishi wa Kampuni ya Avomeru Bw. Jesse Oljange kuhusu ukamuaji wa mafuta mbalimbali ikiwemo ya zao la parachichi katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.