Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezungumza na wananchi wa Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Ijumaa Februari 28, 2025 Uwanja wa CCM Mkwakwani, akieleza maono yake makubwa kwa maendeleo ya mkoa huo.

Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Pia ametoa hakikisho kwa wananchi wa Tanga kuwa serikali imejipanga kujenga barabara ya Bagamoyo โ€“ Pangani โ€“ Tanga kwa kiwango cha lami, pamoja na kuanza upembuzi yakinifu wa barabara ya Segera โ€“ Tanga kwa upanuzi wa baadaye.

Kuhusu sekta ya maji, Rais Samia amesema upatikanaji wa maji umefikia asilimia 80 kwa wastani, na miradi mikubwa miwili inayoendelea itapandisha upatikanaji wa maji mjini hadi asilimia 95 na vijijini hadi asilimia 90.

Akizungumzia maendeleo ya bandari, Rais Samia ameeleza kuwa mizigo imeongezeka kutoka tani 400,000 hadi tani 1,200,000, hali ambayo imeongeza ajira kwa vijana wa Tanga.

Amebainisha kuwa serikali ina mpango wa kuifanya bandari ya Tanga kuwa kituo maalum cha usafirishaji wa mbolea na mazao ya kilimo ili kuongeza ajira zaidi.

Katika sekta ya viwanda, Rais Samia amesema tayari amezindua kiwanda cha chokaa na saruji cha Maweni Limestone Ltd, ambacho baada ya upanuzi wake kimeongeza ajira 824, kati ya hizo 424 ni za kudumu na 400 zisizo za kudumu.

Kwa upande wa kilimo, Rais amesisitiza kuongeza uzalishaji wa korosho, cocoa na viungo, akieleza kuwa mazao hayo yana soko kubwa duniani na ni fursa muhimu kwa vijana.

Katika sekta ya mawasiliano, ametangaza kuwa mradi wa kuimarisha usikivu wa redio ya Taifa katika wilaya za Kilindi, Lushoto na Mkinga umefikia asilimia 60, huku serikali ikiendelea na ujenzi wa minara 758 katika mikoa 26 kwa gharama ya bilioni 126.

Aidha, Rais Samia ametangaza kuwa serikali imechukua ombi la kuanzisha chuo kikuu mkoani Tanga, na tayari kupitia Mradi wa HEET, Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe itajengwa wilayani Mkinga.

Amesisitiza umuhimu wa utalii wa fukwe, historia na utamaduni katika mkoa wa Tanga, akieleza kuwa vivutio kama Mapango ya Amboni, Magofu ya Pangani, Msikiti wa Kale na kumbukumbu za Shaaban Robert vinaweza kuifanya Tanga kuwa kituo kikubwa cha utalii.

Katika kumalizia, Rais Samia amewahimiza wananchi wa Tanga kuchangamkia fursa zinazotokana na maendeleo yanayoletwa na serikali, huku akiwahimiza kushiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Oktoba 2025.

Amemalizia kwa kuwatakia wananchi wa Tanga mfungo mwema wa Ramadhani na Kwaresma, akiwatakia baraka na mafanikio katika kipindi hiki muhimu.

About Author

Bongo News

4 Comments

    I greatly appreciate your ability to convey complex ideas in a comprehensible manner. Well done!

    o8s82e

    Wohh exactly what I was searching for, thankyou for putting up.

    I think other website proprietors should take this site as an model, very clean and great user friendly style and design, let alone the content. You are an expert in this topic!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *