KITAIFA

RAIS SAMIA ATEMBELEA BUNGE LA MALAWI, AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA RAIS WA KWANZA WA NCHI HIYO HAYATI KAMUZU BANDA

RAIS SAMIA ATEMBELEA BUNGE LA MALAWI, AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA RAIS WA KWANZA WA NCHI HIYO HAYATI KAMUZU BANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Malawi na Baba wa Taifa hilo Hayati Dkt. Kamuzu Banda lililopo katika Makumbusho ya Kamuzu, Lilongwe nchini Malawi tarehe 6
Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Cecilia Kadzamira ambaye alifanya kazi kwa karibu na Rais wa Kwanza wa Malawi na Baba wa Taifa hilo Hayati Dkt. Kamuzu Banda wakati alipokuwa akitoka kwenye Makumbusho ya Kamuzu, Lilongwe nchini Malawi tarehe 6 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Bunge la Malawi zilizopo Jijini Lilongwe tarehe 6 Julai, 2023. Kulia ni Makamu wa Rais wa Malawi Dkt. Saulos Klaus Chilima akiwa pamoja na Spika wa Bunge hilo Bi. Fiona Kalemba kushoto.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti nje ya Ofisi za Bunge la Malawi kama kumbukumbu wakati alipofanya ziara Ofisini hapo Jijini Lilongwe nchini Malawi tarehe 6 Julai, 2023.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *