KITAIFA

RAIS SAMIA ATEUA MABALOZI

RAIS SAMIA ATEUA MABALOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi
wa Mabalozi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi. Kabla ya
uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la
Wanamaji (JWTZ).
ii) Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo
Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).
iii) Amemteua Bw. Mohamed Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu
alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.
iv) Amemteua Bw. Gelasius Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw.
Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.
v) Amemteua Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt.
Abdallah alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.
vi) Amemteua Bw. Hassan Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw.
Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala,
Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.
vii) Amemteua Bw. Imani Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw.
Njalikai alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu –
Hotuba
viii) Amemteua Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw.
Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.

Uteuzi huu wa Mabalozi umeanza tarehe 10 Mei, 2023 na wataapishwa kwa tarehe
itakayopangwa baadae.

About Author

Bongo News

69 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *