KITAIFA

RAIS SAMIA ATOA BILIONI 4 UJENZI WA SOKO LA KISASA NZEGA PARKING

RAIS SAMIA ATOA BILIONI 4 UJENZI WA SOKO LA KISASA NZEGA PARKING
  • Atoa mitaji kwa wajasiriamali na Wafanyabiashara wa soko hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la kisasa la Nzega Parking mkoani Tabora Ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.

Rais Dkt, Samia ametoa fedha hizo alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko Hilo.

Aidha Rais Samia amewataka Wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *