KITAIFA

RAIS SAMIA AWAASA WANAWAKE KUSIMAMIA MAADILI YA JAMII

RAIS SAMIA AWAASA WANAWAKE KUSIMAMIA MAADILI YA JAMII

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka
wanawake kushikamana na kuilea jamii katika malezi yaliyo bora kimaadili ili
kuiepusha jamii na vitendo viovu.
Rais Samia ametoa tamko hilo leo katika kongamano la wanawake wa Kiislam
Zanzibar mwezi 27 katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu 1445 – Hijjiria
lililofanyika ukumbi wa Golden Tulip.
Aidha, Rais Samia amesema kila mwanamke ana wajibu wa kusimamia maadili kwa
kuwa ana mchango mkubwa sana katika kujenga au kumomonyoa maadili ya familia
na jamii kwa ujumla.
Vile vile, Rais Samia amesema hivi sasa wanawake wamekuwa mstari wa mbele
kupigania haki na kushiriki katika masuala ya kitaifa na kijamii kwa kufanya kazi
kwa uadilifu, uhakika na weledi mkubwa ambazo awali walidhaniwa hawaziwezi.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wanawake kujiepusha na vitendo vya
unyanyasaji kwa kuwa vinarejesha nyuma maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Rais Samia pia amesema ukosefu wa elimu ya msingi ya dini unaathiri jamii na
kusababisha vitendo vinavyokiuka maadili kama udhalilishwaji wa kijinsia, wizi na
matumizi ya dawa za kulevya na kuliondoshea taifa heshima, haiba na kuua vizazi
vyetu.
Hali kadhalika, Rais Samia amewasihi wanawake kujiendeleza kielimu na kujitokeza
kutumia fursa za kimaisha kila zinapojitokeza ili waweze kuinusuru jamii kwa
kupambana na changamoto zinazojitokeza.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *