KITAIFA

RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUTAFUTA FURSA

RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUTAFUTA FURSA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Jaji Mhe. Sivangilwa Mwangesi kwenye picha ya kumbukumbu na Mabalozi Wateule aliowaapisha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewataka Mabalozi kufuatilia utekelezaji wa Mikataba na Hati za Makubaliano
zinazotokana na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi.
Rais Samia ametoa tamko hilo leo katika hafla ya kuwaapisha Mabalozi wateule
iliyofanyika Ikulu, Chamwino.
Aidha, Rais Samia amesema ufuatiliaji huo uende sambamba na utekelezaji wa
makubaliano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali yanayotokana na Tume za Pamoja
za Ushirikiano na Mashauriano ya Kidiplomasia.
Vile vile, Rais Samia amewataka Mabalozi kuibua masuala ya ushirikiano katika
vituo vyao vya kazi na kutafuta fursa mbalimbali ikiwemo katika sekta ya uwekezaji,
utalii pamoja na mahitaji ya ‘diaspora’.
Rais Samia pia amewataka Mabalozi kufanya kazi kwa kuzingatia Dira ya Ajenda za
Maendeleo za kimataifa na kitaifa ikiwemo falsafa ya 4Rs (Maridhiano, Ustahamilivu,
Mabadiliko na Kujenga Upya) kwa maslahi ya taifa.
Kwa upande mwingine, Rais Samia ameielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaandaliwa mfumo
utakaoingiza maelekezo ya ziara za viongozi wa ndani na nje ya nchi.
Rais Samia ameongeza kuwa mfumo huo utaonesha jukumu la kila wizara kwenye
makubaliano yaliyofikiwa ili kuweza kupima utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *