KITAIFA

RAIS SAMIA KUWAREJESHEA ZAIDI YA HEKTA 74000 WANANCHI WA MBARALI BAADA YA MGOGORO WA MIAKA SABA KUISHA

RAIS SAMIA KUWAREJESHEA ZAIDI YA HEKTA 74000 WANANCHI WA MBARALI BAADA YA MGOGORO WA MIAKA SABA KUISHA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa Akizungumza katika kikao cha pamoja  baina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Wabunge wa Mbarali, Uongozi wa CCM wilaya ya Mbarali  na Uongozi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) kilichofanyika eneo la Kapunga kata ya Itamboleo  wilayani Mbarali .

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inakwenda kurejesha   hekta 74,432 kwa wananchi wa Mbarali  zilizokuwa Eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha  baada  ya zoezi hilo la kuziomba kushindikana kwa takribani miaka saba ili zitumike  katika shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwa  ni pamoja na ufugaji na kilimo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa katika kikao cha pamoja  baina Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Wabunge wa Mbarali, Uongozi wa CCM wilaya ya Mbarali  na Uongozi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) kilichofanyika eneo la Kapunga kata ya Itamboleo  wilayani Mbarali na baadaye kuelekea kwenye maeneo ya mipaka yenye  migogoro na kuongea na wananchi wa maeneo hayo Juni 22 mwaka huu.

Mhe. Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa  migogoro yote ya mipaka  inamalizika kwa  haraka  ili lengo la kuhifadhi raslimali maeneo hayo  na raslimali za taifa na kuboresha maisha ya wananchi yanafikiwa.

Amesema katika kipindi hiki kifupi cha Serikali ya mama Samia  tayari maeneo mengi yameshafikiwa na  kutatua  migogoro ya mipaka  iliyodumu kwa muda  mrefu ikiwa ni pamoja na eneo vijiji vya Tarime  vinavyozunguka  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo amewaomba wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na Serikali yao  katika kutatua  migogoro hiyo  kwa  kuwa  hakuna jambo  linaloshindikana.

Aidha, amewaomba wananchi  kutambua kuwa  maeneo  yaliyotengwa kwa uhifadhi  yana umuhimu mkubwa  kwa  shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa kuwa ndiyo  vyanzo vya  maji yanayokwenda  kwenye  bwawa la umeme la Mwalimu  Nyerere ambalo ndilo  chanzo kikuu cha uzalishali wa umeme kwa taifa letu.

Akiwapitisha kwenye andiko la tathmini ya eneo hilo Mjumbe wa Kamati ya  Mkoa wa Mbeya ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa uwekaji wa mpaka unaoendelea katika wilaya za Mbarali na Chunya mkoani Mbeya Kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya  Syabumi Mwaipopo ameiambia kamati na  viongozi wote waliofika  katika kikao hicho kuwa kamati ilizingatia mambo mbalimbali  wakati wa kufanya tathmini  hiyo ili iwe na gtija na iendane na uhalisia.

Ameyajata  baadhi ya mambo yaliyozingatiwa kuwa ni  pamoja na mwinuko  kutoka usawa wa bahari, uoto wa mimea, uwepo wa ardhi oevu na shughuli  za kibinadamu zenye athari za  kimazingira ambapo  pia alisema  mapendekezo ya maboresho ya GN 28  yalikuwa ni shamba la madibila phase 2 libaki katika hifadhi wakati Madibila  phase 1  liachwe huru kwa wananchi, eneo  la NARCO litolewe ndani ya Hifadhi  na vijiji  vitano  pekee badala ya kumi na sita vya awali  wapishe  hifadhi.

Akizungumzia kuhusu madai yay a Shamba la Kapunga kutopitiwa  na mipaka mipya   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera amefafanua  kuwa shamba hili halikupitiwa na GN 28 mpya  kwa sababu GN mpya inapita katika maeneo yale yale yaliyopitiwa na GN.28 na wala haianzishi maeneo mapya ambayo hata ile ya awali haikupitiwa.

Hata, hivyo wananchi watambue kuwa Kapunga Estate ni shamba la serikali na huyu mwekezaji amepewa awekeze tu kwa muda maalum, na mkataba wake utakapoisha shamba hili litarudi serikalini.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe.Timotheo Paul Mnzava alisema kamati  hii ya Bunge  inasimamia shughuli za Maliasili na Ardhi kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  hivyo basi msingi wa safari hiyo ni kujiridhisha ili kulishauri Bunge kuona namna bora  kumaliza hili jambo.

Aidha, mwenyekiti huyo aliongeza kuwa nchi ni yetu sote lazima tulinde wananchi wetu na pia tulinde Maliasili zetu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Amesema kuwa baada ya kamati hii kutembelea uwandani na kujionea hali halisi itawasilisha mapendekezo ya walichokiona bungeni ili kubadili GN.28 na kuja na GN. mpya ambayo itakuwa ni suluhu kwa mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 18.

About Author

Bongo News

1 Comment

    I think you have observed some very interesting details, appreciate it for the post.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *