Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Februari 25, 2025 anaingia siku yake ya tatu ya ziara yake ya Kikazi Mkoani Tanga, akitarajiwa kuzindua shule ya Sekondari ya wasichana Tanga na baadae kutembelea na kuzindua Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Kilindi kando ya kuzungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Kulingana na taarifa za serikali, Shule ya sekondari Tanga ilitengewa bajeti ya takribani Bilioni tatu za ujenzi, lengo likiwa likiwa ni kuweka mazingira rafiki kwa watoto wa kike kuweza kupata elimu bora sambamba na kuhamasisha na kuchochea wasichana kupenda na kuchagua kusoma masomo ya Sayansi.

Rais Samia Suluhu Hassan pia anatarajiwa leo kufungua Jengo la Halmashauri ya Mji wa Handeni na kusalimia wananchi wa Halmashauri ya Handeni ambalo serikali imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 4.2 kwaajili ya ujenzi wake, Jengo ambalo lina sehemu za hoteli, kumbi za mikutano na sehemu za kukodisha kwa taasisi za kifedha.

Rais Samia pia kulingana na ratiba yake Mkoani Tanga, ataweka jiwe la msingi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji wa Miji 28 uliopo mtaa wa Vibaoni wilayani Handeni.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa ziarani Mkoani humo kwa siku ya tatu hii leo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kushika usukani wa kuwa Rais wa Tanzania amenukuliwa mara kadhaa akisema kuwa lengo kuu la Ziara yake ni kukagua thamani ya fedha na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotokana na zaidi ya Shilingi Trilioni 3.1 ambazo zimetolewa na serikali kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

About Author

Bongo News

2 Comments

    vzrjrd

    Hey, I think your blog might be having browser compatibility issues. When I look at your blog site in Firefox, it looks fine but when opening in Internet Explorer, it has some overlapping. I just wanted to give you a quick heads up! Other then that, amazing blog!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *