
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Novemba 19,2023 ameshiriki IFM Alumni Marathon ambayo imeandaliwa na Watumishi na Wanafunzi waliosoma katika chuo hicho cha Usimamizi wa fedha ambao kwa sasa wanafanya kazi maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akiongea mara baada ya kukimbia umbali wa kilometa 5 Mhe. Chalamila amekipongeza chuo hicho kwa kubuni matembezi hayo ambayo mapato yanayopatikana yanatumika katika maendeleo ya Chuo.
“Jambo linalofanywa na IFM ni la Kizalendo nitoe rai kwa vyuo vingine kuiga mfano huo wa kibunifu ambao una masilahi mapana sio tu kwa chuo bali hata Taifa kwa ujumla” Alisema RC Chalamila

Aidha amewataka kufanya maboresho katika matembezi hayo kwa kushirikisha makundi mengi zaidi kwa mfano kundi la jogging ili kuweza kusambaza ujumbe ufike mbali zaidi, vilevile ametoa Salamu za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo amesema Rais anawasalimu na anafurahishwa na kitendo hiki cha kutambua umuhimu wa mazoezi katika Afya ya Binadamu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja huo alishiriki mbio hizo kwa umbali wa kilomita 5.
Dkt. Yonazi amesema kuwa marathon hiyo imehusisha watu ambao walisoma IFM, na marafiki ili kuleta umoja wa wana IFM na kuongezea kuwa mbio hizo huchangia maendeleo ya Chuo na Taifa, pia amewashukuru wadhamini wote waliojitoa kwa hali na mali kuwezesha kufanyika kwa mbio hizo.

Naye Mkamu Mkuu wa chuo hicho Dkt. Mnzava amemshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwa kuungana nao katika mbio hizo ambapo amesema ni tukio la kihistoria na ni mara ya kwanza toka chuo kianze mwaka 1972, amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuendeleza mbio hizo, kwa kuhamasisha makundi mbalimbali kushiriki kwa kuwa mazoezi ni Afya kama kauli mbiu inavyosema ” Badili Mwenendo Wako wa Maisha kwa Afya Bora”

11 Comments
Thanks – Enjoyed this post, is there any way I can receive an update sent in an email when you publish a fresh article?
8qkp9h
It is actually a great and helpful piece of information. I am happy that you simply shared this useful info with us. Please keep us informed like this. Thank you for sharing.
F*ckin’ remarkable things here. I am very glad to peer your article. Thanks a lot and i am taking a look ahead to contact you. Will you please drop me a mail?
zsse9v
I like this weblog very much so much fantastic information.
Can you be more specific about the content of your article? After reading it, I still have some doubts. Hope you can help me.
Nice post. I was checking continuously this blog and I’m impressed! Extremely useful information particularly the last part 🙂 I care for such info much. I was looking for this particular information for a very long time. Thank you and best of luck.
Situs Slot Online yang Menjamin Keuntungan Maksimal, cari di SIGMASLOT
Situs Slot Online yang Menjamin Keuntungan Maksimal, cari di SIGMASLOT
Situs Slot Online yang Menjamin Keuntungan Maksimal, cari di SIGMASLOT