-Ataka kutekelezwa haraka kwa maelekezo yake ili kufikia adhima ya serikali kufanya biashara saa 24
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 10,2024 amefanya kikao na viongozi wa wafanyabiashara pamoja na viongongozi wa Serikali, Taasisi, Mashirika na wataalam kutika ofisi yake katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazi mmoja Wilaya ya Ilala Jijini humo.
RC Chalamila amesema Soko la Kariakoo ni Soko la Kimataifa na Serikali imefanya na inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa,ambapo ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 28 ni moja ya ushaidi tosha wa uwekezaji huo.
Aidha RC chalamila ameagiza kufanyika kwa yafuatayo: mosi kuanza kupendezesha Soko la Kariakoo,kuweka mazingira yanayovutia ikiwemo kuwapanga vizuri wafanyabiashara hususani wadogowadogo,pia usafi wa mazingira uoendana na kuweka vizuri mifumo ya maji taka na usafi kwa ujamla wake ambapo amesema wakandarasi wenye uwezo na vifaa vya kisasa ndiyo wanatakiwa.
Vilevile DART ambaye ni msimamizi wa huduma za mabasi ya haraka kuweka mkakati kabambe wa kuhakikisha mabasi hayalali yanafanya kazi saa 24, pia katika ukanda wa Kariakoo kuanzisha Kituo cha pamoja cha kutoa huduma kwa wafanyabiashara, lakini kwa upande wa LATRA RC Chalamila ameitaka kuangalia Route za mabasi yanayo kuingia na kutoka ukanda wa kariakoo.
Sanjari na hilo RC Chalamila amezitaka taasisi na mashirika katika mkoa huo kuchangia taa za barabarani ili kuwezesha usalama nyakati zote, pia kufungwa CCTV Camera aidha amewataka vyombo vya dola kijipanga vizuri kuimarisha ulinzi na usalama saa 24.
Sambamba hilo Mhe Mkuu wa Mkoa ameagiza uhamiaji kufanyia kazi wageni wanajishughulisha na kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa vilevile taasisi za fedha kuanza kujipanga kuwa na dirisha la kutoa huduma hiyo saa 24 vilevile TANROAD, TARURA kuhakikisha barabara za ukanda wa soko la kariakoo zinakuwa nzuri bila mashimo “ Rais Samia matarajio yake ni kuona watu wengi wanakuwa busy na mifumo ya biashara” Alisama Chalamila.
Mwisho Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kusimamia kwa weledi mkubwa maelekezo yake kwa masilahi mapana ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.