KITAIFA

RC CHALAMILA MARUFUKU WAZAGAAJI, WATOTO WA MTAANI NA OMBAOMBA BARABARANI

RC CHALAMILA MARUFUKU WAZAGAAJI, WATOTO WA MTAANI NA OMBAOMBA BARABARANI

– Asema Serikali imewekeza zaidi ya Trilioni 3 kwenye vituo vingi vya kulelea walemavu ikiwemo Dar es Salaam

– Imebainika kuwa Ulemavu kwa sasa ni Mtaji

-kuhusu Kamata kamata ya magari ya takataka aitisha Kikao Kati yake na wadau husika kitakachotoa maelekezo ya pamoja kuhusu hilo

– Dar es Salaam ni Mji wa  Kibiashara hivyo Ugonjwa wa Kipindupindu hautakiwi kupenyeza kabisa

-Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wapokea maagizo na kuahidi kuyafanyia kazi

-Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Mohamed Mang’una aelezea nini kifanyike kuuepuka Ugonjwa huo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Januari 15, 2024 amepiga MARUFUKU uzagaaji wa watu kwenye maeneo yote ya msingi Kama vile Tanzanite bridge na Ubungo, watoto wa mitaani  na Ombaomba barabarani ambapo amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuwafukuza na wengine kuwakamata

Ameyasema hayo katika Mkutano wake na Watendaji wa Serikali uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Jubilee Uliohusu tahadhari dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko

RC Chalamila amesema Serikali imewekeza zaidi ya Tirioni 3 kwenye vituo vingi vya kulelea walemavu Nchini ambapo Dar es Salaam Kuna kituo kikubwa Cha kulelea walemavu pia

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Imebainika kuwa Ulemavu kwa sasa Ni Mtaji ambapo wale ambao sio walemavu huenda kuwakusanya walemavu Kisha kuwatembeza kwenye baiskeli ambapo Jioni huchukua kilichokusanywa na walemavu hao na kuwapatia walemavu hao kiasi kidogo Cha pesa Kati ya Tsh 3000 mpaka Elfu 5000 kwa siku

Kuhusu Kamata Kamata ya magari ya takataka RC Chalamila ameitisha Kikao Kati yake na Mwenyekiti wa wakandarasi, kundi dogo la wakandarasi, ZPC, ZTO ili baada ya Kikao hicho yatolewe maelekezo ya pamoja yatakayosaidia magari hayo kwenda kwa haraka

Dar es Salaam ni Mji wa Kibiashara hivyo Ugonjwa wa Kipindupindu hautakiwi kupenyeza kabisa na ndio maana amewaita wadau kusaidia upatikanaji wa vifaa vya Usafi, Wakuu wa Wilaya kuhakikisha Watendaji wanasimamia Usafi kufanyika kila wiki, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi kuhakikisha uchafu haukai sehemu muda mrefu, Ras na Wakuu wa Wilaya kuendesha dampo kwa ubia na ulipaji wa ushuru bila shuruti

Kwa upande wao, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wakili kupokea maagizo yote na kuahidi kuyafanyia kazi

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohamed Mang’ una ameeleza Nini kifanyike ili Kudhibiti Ugonjwa huo kuwa ni:-
– Halmashauri kutoa Elimu endelevu ya kanuni  Bora za Afya katika ngazi zote
– Dawasa kuendelea kutibu maji yanatumiwa na jamii
-Uondoshwaji wa taka ufanyike kwa wakati
-Kuepuka ulaji wa vyakula vilivyoandaliwa katika mazingira machafu
– wananchi kuchemsha maji
-Wananchi kuizingatia Usafi na usafi wa mazingira
– kula chakula Cha Moto
-Vyakula vilivyopikwa vihifadhiwe vizuri
– kuosha matunda kwa maji Safi na salama

*#Ikumbukwe kuwa RC Chalamila atagawa Vifaa  vya usafi tarehe 20 Hadi 21 Januari, 2024 kwenye Vyombo vya dola*

About Author

Bongo News

5 Comments

    セックス ドール今すぐウェブサイトを訪れて、その違いを体験してみてください—あなたの素晴らしいドールを手に入れる旅が今、始まります!熟練のコレクターでも、新たにリアルドールの世界に足を踏み入れた方でも、comはあなたに長年にわたる喜びと満足感をもたらす完璧なコンパニオンを見つける場所です.comは、リアルドールの選択肢が豊富で、ユーザーにとって魅力的なオプションを提供することで、業界内で特に高い評価を得ています.

    Грузоперевозки Новосибирск с попутным грузом – это ваш путь к экономии https://vk.com/gruz_poputno

    Подписывайтесь на @android_1xslots и активируйте промокод LEGAL1X для получения бонусов в 1xSlots https://t.me/android_1xslots

    Скачайте APK для 7k Casino и активируйте промокод ANDROID777, который доступен в телеграм канале https://t.me/casino_7kk

    https://t.me/s/kino_film_serial_online_telegram 862702 лучших фильмов. Фильмы смотреть онлайн. В нашем онлайн-кинотеатре есть новинки кино и бесплатные фильмы самых разных жанров

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *