KITAIFA

RC MAKONDA AANZA KUMJENGEA NYUMBA BIBI PENINA.

RC MAKONDA AANZA KUMJENGEA NYUMBA BIBI PENINA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameanza utekelezaji wa ahadi yake ya Kumjengea Bibi Penina Petro (70) Vyumba vitatu na sebule huko Siwandete Kata ya Kiranyi wilayani Arusha.

Mhe. Mkuu wa mkoa aliahidi kumjenga nyumba Bibi huyo wakati wa kliniki yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Arusha na ndipo bibi huyo alipoanza kulia na kueleza masaibu ya nyumba yake kudondoka na ndugu zake kugoma kumjengea nyumba mpya kutokana na kutojaliwa kupata mtoto na hivyo kudai kuwa hakuna haja ya kumjengea nyumba mpya kwani hana muda mrefu wa kuendelea kuishi duniani.

Tayari wataalamu wa ujenzi wamefika kwenye eneo la bibi huyo kwaajili ya upembuzi wa awali na kupima eneo hilo na kulingana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ujenzi wa nyumba hiyo unatarajiwa kuanza wiki hii.

Bibi Penina ametumia fursa hiyo kumuombea kheri na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali wanyonge na kuwa majibu ya changamoto zao huku pia akimshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa Paul Christian Makonda kwa kuja na kliniki ya kuwasikiliza na kutatua changamoto za wananchi pamoja na kuwa na nidhamu katika kuahidi na kutekeleza.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *