KITAIFA

SACCOS YA JKCI KUTOA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 20

SACCOS YA JKCI KUTOA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 20

Mwenyekiti wa JKCI SACCOS Dkt. Tulizo Shem akizungumza na
wanachama wa SACCOS hiyo wakati wa mkutano mkuu uliofanyika hivi karibuni
kupitia taarifa za fedha za mwaka 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi
hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mfuko wa SACCOS ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ina
uwezo wa kukopesha wanachama wake hadi kiasi cha shilingi milioni ishirini
endapo mwanachama atakidhi vigezo na masharti vilivyowekwa na SACCOS hiyo.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa SACCOS hiyo ambaye ni Daktari bingwa wa
magonjwa ya moyo wa JKCI Tulizo shem alipokuwa akizungumza na wanachama
wa SACCOS hiyo hivi karibuni wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa
Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mwanachama wa JKCI SACCOS Maangaza Omary akichangia mada wakati
wa mkutano mkuu wa SACCOS hiyo uliofanyika hivi karibuni kupitia taarifa za
fedha za mwaka 2022 katika ukumbi wa mikutano wa JKCI iliyopo jijini Dar es
Salaam.


“Sasa hivi SACCOS yetu inauwezo wa kumpa mwanachama wake mkopo wa
shilingi milioni ishirini endapo mwanachama huyo hisa zake zinauwezo wa kulipa
rejesho la mkopo wake”, alisema Dkt. Shem
Akizungumzia muda wa kupata mkopo Dkt. Shem alisema kwa sasa mwanachama
anaweze kupata mkopo ndani ya muda wa nusu saa endapo kama atakamilisha
maombi ya mkopo kwa wakati.
“Mwanachama wa JKCI SACCOS anaweza kupata mkopo wake ndani ya dakika
thelathini na atalipa marejesho yake ndani ya miezi tisa badala ya miezi sita kama
ilivyokuwa hapo awali, tunafanya hivi ili wanachama wetu waweze kufanya
maendeleo kupitia mikopo wanayochukua”, alisema Dkt Shem.

Wanachama wa JKCI SACCOS wakifuatilia wakati wa mkutano mkuu wa
SACCOS hiyo uliofanyika hivi karibuni kupitia taarifa za fedha za mwaka 2022
katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.


Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Mkurugenzi wa Idara ya Tiba ya Moyo Dkt. Tatizo Waane alisema wajumbe
wa bodi wa SACCOS ya JKCI wanatakiwa kuangalia fursa mbalimbali zilizopo katika
mazingira ya JKCI na kuzitumia kama chanzo cha kutunisha mfuko wa chama kwa
kuwekeza katika fursa hizo.
“Wajumbe wa bodi ya SACCOS ya JKCI mnaweza kuwekeza katika usafi na
mgahawa huduma zinazotolewa hapa ndani ya JKCI, kama SACCOS itawekeza
katika maeneo haya Taasisi itakuwa inailipa Saccos na mapato ya SACCOS
yataongezeka”, alisema Dkt. Waane
Dkt. Waane alisema kwa sasa JKCI baada ya kupewa hospitali ya Dar Group idadi
ya wafanyakazi imeongezeka hivyo ni wakati sasa viongozi wa SACCOS hiyo

kufikisha taarifa kwa wafanyakazi hao ili nao waweze kuwa sehemu ya Saccos
hiyo na kunufaika na mikopo inayotolewa.

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Muhimbili Frank Makungu akizungumza
na wanachama wa JKCI SACCOS wakati wa mkutano mkuu wa SACCOS hiyo
uliofanyika hivi karibuni kupitia taarifa za fedha za mwaka 2022 katika ukumbi wa
mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.


“Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwani Novemba mwaka jana iliikabidhi
JKCI hospitali ya Dar Group hivyo wafanyakazi wa Dar group nao waambiwe
umuhimu wa kujiunga na SACCOS hii kuongeza idadi ya wanachama lakini pia
kuikuza SACCOS”, alisema Dkt. Waane.
Naye Meneja wa Benki ya NMB tawi la Muhimbili Frank Makungu alisema SACCOS
ya JKCI ina muda mfupi lakini inamafanikio makubwa hivyo kuwataka wanachama
wa SACCOS hiyo kufuata masharti yaliyowekwa kuifanya SACCOS hiyo kuendelea
kuwa katika ubora wake.
“Nimekuwa nikishauriana na viongozi wa SACCOS hii kuhusu mambo mbalimbali,
leo nawashauri wanachama mkope kwenye SACCOS yenu, mlipe kwa wakati na
muwe mabalozi wazuri wa kuisema vema SACCOS yenu kwa wengine kwani
kwakufanya hivyo SACCOS yenu itakuwa”, alisema Makungu.
Akizungumzia uzoefu alionao katika vyama vya mikopo Afisa Ushirika Ofisi ya
Msajili Msaidizi Olivia Kaiza alisema SACCOS nyingi zinashindwa kuendelea kwa
sababu ya kutegemea posho katika kukata mapato ya Mfuko hivyo kuitaka JKCI
kuhusisha mishahara kulipa mkopo kuliko kutegemea posho.
“Posho ni fedha ya ziada ambayo inaweza kusitishwa wakati wowote, nawashauri
wajumbe wa bodi ya JKCI SACCOS kutotegemea posho kukata riba za mikopo bali
mikopo ikatwe kwenye mishahara maana mshahara ni lazima mtu apate”, alisema
Oliva.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *