Rais Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Brazil jana kuhudhuria mkutano wa Nchi Tajiri Duniani wa G20 imealikwa kwa mara ya kwanza.

Nchi wanachama wa G20 zinamiliki asilimia 85 ya uchumi wa dunia na Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini duniani. Ni kwa nini Tanzania imealikwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Noel Kaganda, mambo matatu yameipaisha Tanzania. Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Rio de Janeiro jana, Kaganda alizitaja sababu hizo kuwa ni;

Mosi ajenda ya nishati. Rais Samia amejipambanua kama kama mzungumzaji na mtetezi kinara wa matumizi ya nishati safi duniani. Suala la nishati litajadiliwa kwa kina kwenye mkutano huo na Rais wa Brazil, Lula da Silva, ambaye ndiye mwenyeji wa G20 mwaka huu, amemwalika Rais Samia kwa kuzingatia hilo.

La pili ni kuhusu vita dhidi ya njaa na umasikini. Ajenda kubwa ya Brazil kwenye mkutano huu inahusu kuondoa njaa na umasikini. Hili ni eneo lingine ambalo Rais Samia analifanyia kazi kwa karibu. Mwaka jana alikuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa mifumo ya chakula uliofanyika na Dar.

Mkutano unazungumzia dunia yenye haki, usawa na maendeleo endelevu. Kama Rais mwanamke kutoka kwenye nchi zinazopambania mifumo yenye haki duniani na championi wa maendeleo endelevu, Rais Samia ana sifa za jumla zinazoendanana na ajenda na muktadha wa G20 mwaka huu.

About Author

Bongo News

31 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *