Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akihimiza jambo kwa walimu wa Shule ya Msingi ya Segesa ya wenye uhitaji maalum na watendaji wa Manispaa ya Kahama, mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Dkt. Charles Msonde amesema Serikali haitomsamehe yeyote
atakayebainika kukwamisha ujenzi wa miundombinu ya elimu katika shule
za Sekondari na msingi.
Dkt. Msonde amesema hayo kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Msalala,
Ushetu na Kahama Manispaa kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya
miundombinu ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri hizo.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akisisitiza jambo wakati akikagua moja ya darasa linalojengwa katika Shule ya Msingi Bulyanhulu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
“Serikali haitomsahe yeyote atakayesababisha wanafunzi wakose mabweni
na madarasa wakati imetoa kwa wakati fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu hiyo ya elimu,” Dkt. Msonde amesisitiza.
Ili kuhakikisha miundombinu ya elimu inakamilika kwa wakati, Dkt. Msonde
amezitaka menejimenti za halmashauri hizo kuongeza mafundi wenye
uwezo wa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu katika shule za
sekondari na msingi ili wanafunzi wapate mazingira bora ya kupata elimu.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akikagua uimara wa ukuta wa darasa linalojengwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tinde, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Ameongeza kuwa, ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu kupitia mradi wa
BOOST ilikuwa imepewa muda maarumu wa kukamilika, hivyo amewataka
viongozi wa halmashauri zote nchini kuhakiksha ndani ya siku 10
wanakamilisha miundombinu hiyo ili iweze kutumiwa na wanafunzi.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akisalimiana na mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Bulyanhulu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa mradi wa miundombinu ya elimu.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga ambaye ni
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako amesema, ofisi
yake itahakikisha watendaji wa halmashauri zote zinazoteleza Mradi wa
BOOST katika eneo lake la utawala, wanafanya kazi usiku na mchana ili
kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu.