Uncategorized

SERIKALI ITAJENGA MAGHALA YA CHAKULA NCHI NZIMA-SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema
Serikali imepanga kununua chakula na kuweka akiba katika maghala kwa kiasi cha
tani laki tano kwa mwaka huu ikilinganishwa na tani laki mbili na hamsini kwa mwaka
uliopita.
Rais Samia ameyasema hayo leo katika Tamasha la Utamaduni la Bulabo ambalo ni
sherehe za kumshukuru Mungu kwa mavuno lililofanyika katika uwanja wa Red
Cross Ngomeni uliopo Kisesa.
Aidha, Rais Samia amesema Serikali itajenga maghala ya chakula katika kila mkoa ili
kuweza kuhifadhi chakula kitakachoweza kuhudumia wananchi katika kila mkoa.
Rais Samia pia amesema Serikali imejipanga kuhakikisha nchi inakuwa na chakula
cha kutosha kwa kuongeza matumizi katika sekta ya chakula ikiwemo kuongeza
fedha kwenye bajeti ya kilimo ili wananchi waweze kuzalisha ziada ya chakula.
Vile vile, Rais Samia amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kujenga skimu za
umwagiliaji ili wakulima walime na kuvuna mara mbili kwa mwaka badala ya
kutegemea mvua.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka Machifu kuhamasisha wananchi
kufanya kazi na kuchangia katika shughuli za maendeleo ili kujenga taifa bora.

About Author

Bongo News

35 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *