KITAIFA

SERIKALI KUKAMILISHA TAFITI ZA MADINI NCHINI

SERIKALI KUKAMILISHA TAFITI ZA MADINI NCHINI
  • Mpaka sasa utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege umefanyika kwa asilimia 16

Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo katika mpango wa kukamilisha utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akihutubia wananchi siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.

Akizungumza juu ya maendeleo ya Sekta ya Madini Mhe.Mavunde alifafanua kuwa Wizara kupitia Dira yake mpya ya 2030 inayosema Madini ni Maisha na Utajiri, imeona katika kuchochea ukuaji wa Sekta ya Madini na kuongeza mchango katika Pato la Taifa, kuna haja ya kupata taarifa za miamba na madini kwa eneo lote la nchi yetu.

Alifafanua kuwa katika kutekeleza dira hiyo pamoja na mambo mengine, Serikali itakamilisha utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege kwa asilimia 100 kutoka asilimia 16 zilizopo kwa sasa ifikapo 2030. Lengo la utafiti huo likiwa ni kuchochea zaidi uwekezaji katika Sekta ya Madini pamoja na kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi.

Maonesho ya Sita ya kimataifa ya Teknolojia ya madini yalifunguliwa rasmi Septemba 23 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na yatafungwa Septemba 30, 2023.

About Author

Bongo News

70 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *