KITAIFA

SERIKALI YAFANYIA UTAFITI MBADALA WA ZEBAKI KWA WACHIMBAJI WADOGO

SERIKALI YAFANYIA UTAFITI MBADALA WA ZEBAKI KWA WACHIMBAJI WADOGO

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis amesema Serikali imefanya utafiti kuhusu teknolojia mbadala
wa zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini.
Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya hatua zilizofikiwa juu ya uratibu
na utekelezaji wa Mpango-kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki
(2020 – 2025) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira.
Kwa mujibu wa Mhe. Khamis, utafiti umeonesha teknolojia za kuchoma
(smelting) kwa kutumia borax na teknolojia za sianadi (cyanidation) ndio
zinatumika kwa wingi nchini na nchi zinazoendelea.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis akiwasilisha taarifa ya hatua zilizofikiwa juu ya uratibu na
utekelezaji wa Mpango-kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki (202
0

  • 2025) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma
    leo tarehe 22 Agosti, 2023. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya
    Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama.


Amesema Mradi wa Kudhibiti Athari za Zebaki kwa Afya ya Binadamu na
Mazingira Kwenye Shughuli za Uchimbaji Mdogo wa Dhahabu Nchini umejikita
katika kufanyia kazi teknolojia zinazotumika zaidi nchini.
”Lengo ni kutekeleza malengo la Mkataba wa Minamata hususan kipengele
cha saba kinachohusu kupunguza matumizi ya zebaki kwenye uzalishaji wa
dhahabu inayozalishwa na wachimbaji wadogo na pale itakapowezekana
kuondoa kabisa matumizi ya kemikali hiyo katika kuzalisha dhahabu kwa
wachimbaji wadogo,” alifafanua.
Pia, Naibu Waziri Khamis alitaja shughuli za mradi kuwa ni kuimarisha na
kujenga uwezo na ujuzi wa taasisi na wachimbaji wadogo kuhusu namna ya
kudhibiti athari zinazotokana na utumiaji wa zebaki kwenye uzalishaji wa
dhahabu.
Aidha, katika kutekeleza Mpangokazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya
Zebaki, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
ikiwemo Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeandaa
Mwongozo wa Uingizaji, Matumizi na Utupaji Salama wa Zebaki.
Mhe. Khamis amesema kuwa Mwongozo huo unalenga kutoa utaratibu wa njia
salama za usimamizi wa Zebaki pasipo kuathiri afya ya binadamu na
mazingira.
Mradi huo wa miaka minne unafadhiliwa na Global Environmetal Facility (GEF)
kwa ruzuku ya Dola za Marekani 7,339,450 sawa na Shilingi za Kitanzania
bilioni 18.3.unatekelezwa katika mikoa saba ya Geita, Mwanza, Mara,
Shinyanga, Singida, Mbeya na Songwe.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *