Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji akizungumza Jijini Dodoma na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika na upande wa kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora imesema itaendelea kuweka mikakati ya kuimarisha uadilifu,
uwajibikaji na utawala bora katika Utumishi wa Umma ili kuleta tija
iliyokusudiwa kwa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji kuzungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw.Cosmas Ngangaji ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati
akizungumza na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha
Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la
kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Amesema Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama hivyo vya Kitaaluma vina
jukumu kubwa la kusimamia dhana ya utawala bora nchini ili kuongeza
uwazi na uwajibikaji zaidi katika Utumishi wa Umma katika kuwahudumia
wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji baada ya kuzungumza nao kwenye kikao kazi na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
“Utawala bora, ni ile dhana inayozingatia maslahi mapana ya taifa, hivyo
ninyi Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma muhakikishe
huduma mnazozitoa zinazingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji, haki sawa,
demokrasia na kuwasikiliza watu wengi na wachache” amesisitiza Bw.
Ngangaji.
Amefafanua kuwa, utaratibu wa kuwakutanisha Wataalamu hao kutasaidia
kutoa mapendekezo ya namna ya kubadilisha na kuboresha Miongozo ya
Usimamizi wa Maadili kwenye Taasisi hizo katika kusimamia dhana ya
utawala bora nchini.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na maafisa waandamizi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amewataka
wasimamizi hao wa maadili kuhakikisha wanawachukulia hatua za
kinidhamu watumishi ambao wanakiuka maadili huku akisisitiza
kuwapongeza na kuwatia moyo watumishi ambao wanafanya vizuri katika
kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika amesema kikao
hicho ni mahsusi kwa ajili ya kubaini changamoto za usimamizi wa maadili
ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kusimamia maadili kutokana na
uzoefu wanaokutana nao.
“Sisi tunaangalia maadili katika masuala ya Utumishi wa Umma lakini kwa
wenzetu waliopo kwenye Vyama vya Kitaaluma wanaangalia madili ya
kitaaluma kwani wapo Watumishi wa Umma ambao ni wanachama wa
vyama hivyo” amesisitiza Bi. Mavika
Akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji, Kaimu
Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Baraza la Uuguzi na Ukunga, Bi.
Jane Mazigo amesema kikao hicho ni muhimu kwao kama wadau muhimu
wa usimamizi na utekelezaji wa maadili ya Utumishi wa Umma katika
Vyama vya Kitaaluma hivyo, anaamini kitatoa mwelekeo mpya katika
kuhakikisha wanabadilishana uzoefu kutokana na changamoto
wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku.