KITAIFA

SIMBACHAWENE AIPONGEZA WHI KWA KUENDELEA KUJENGA MAKAZI BORA YA WATUMISHI, ASISITIZA KUJENGA ZAIDI KARIBU NA MAENEO YA KAZI

SIMBACHAWENE AIPONGEZA WHI KWA KUENDELEA KUJENGA MAKAZI BORA YA WATUMISHI, ASISITIZA KUJENGA ZAIDI KARIBU NA MAENEO YA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Menejimenti ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameipongeza Taasisi ya
Watumishi Housing Investments (WHI) kwa kuendelea kujenga makazi
bora ya watumishi wa umma nchini na kuwasisitiza kuelekeza nguvu
zaidi ya ujenzi jirani na maeneo ambayo watumishi wanafanya kazi ili
kuwaondolea changamoto ya makazi kwa lengo la kuboresha utendaji
kazi.
Mhe. Simbachawene amezungumza hayo jijini Dodoma wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba zilizojengwa na
taasisi hiyo eneo la Njedengwa na Kisasa Relini kwa lengo la kuwauzia
na kuwapangisha watumishi wa umma na wanachama wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiambatana na Naibu Waziri wake, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Bw. Xavier Daudi wakielekea kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.


Mhe. Simbachawene amesema kitendo cha watumishi wa umma
kutokuwa na makazi bora na kuwa mbali na maeneo yao wanayofanyia
kazi ni changamoto kubwa inayoathiri utendaji kazi, hivyo ameisisitiza
taasisi hiyo kuona umuhimu wa kufanya hivyo kwani licha ya kuwasaidia
watumishi kupata makazi bora watakuwa wametekeleza Ilani ya Chama
Cha Mapinduzi na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan ya kuhimiza uwepo
wa makazi bora kwa watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao
kwa ufanisi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.


Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, umuhimu wa kuwa na makazi
bora karibu na maeneo ya kazi, kutawasaidia watumishi hasa
wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza maeneo ambayo yana changamoto
ya nyumba, kutohangaika.
“Mkijenga nyumba maeneo ya jirani na vituo vya kazi, kutawasaidia
sana watumishi hasa wa ajira mpya kutopata changamoto na kuchukia
kazi kwa sababu ya kuhangaika kutafuta sehemu nzuri ya kuishi,” Mhe.
Simbachawene amesisitiza.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameungana na
Mhe. Simbachawene kuipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa

wanayoifanya ya kujenga nyumba bora kwa ajili ya kuwauzia na
kuwapangisha watumishi wa umma na wanachama wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments (WHI) Dkt.
Fredy Msemwa, amewashukuru viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutembelea mradi wa
ujenzi wa nyumba zinazojegwa na taasisi hiyo katika eneo la Kisasa
Relini na Njedengwa na kuhimiza uwajibikaji na ubunifu.
Dkt. Msemwa amewaahidi viongozi hao kuwa, watayafanyia kazi
maelekezo yote ambayo wameyatoa kwa ajili ya kuboresha utendaji
kazi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *