Inbox
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Mwanangwa mara baada ya kukagua Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. George Simbachawene amewapongeza Viongozi na Wananchi
wa Kijiji cha Mwanangwa kwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo
kikamilifu baada ya kuridhishwa na thamani ya fedha iliyotumika katika mradi
wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya
ya Misungwi mkoani Mwanza.
Mhe. Simbachawene ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na
walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha
Mwanangwa, Kata ya Mabuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo
iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF.
“Nimefurahi sana na niwapongeze kwa kusimamia kikamilifu mradi huu wa
ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa uliogharimu
takribani shilingi milioni 168 kupitia fedha za TASAF, nimekagua na kuona
majengo yote yalivyojengwa kwa ufanisi mkubwa, nimeridhika na thamani ya
fedha ambayo imetumika hapa,’’ Mhe. Simbachawene amesema.
Aidha, Mhe. Simbachawene amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa
Misungwi kwa kuchangia nguvu zao katika kufanikisha ujenzi huo, hali
inayoonyesha jamii pia imeshiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule hiyo
itakayowasaidia wanafunzi wa kike kupata elimu bora.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paulo Chacha
amemshukuru Waziri Simbachawene kwa kufanya ziara katika Wilaya yake
na kuahidi kuwa watumishi na wananchi wa Wilaya yake wataendelea
kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano mkubwa ili kuleta maendeleo katika nchi.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Alexander Mnyeti amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kuwapatia fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya
ujenzi wa mabweni ya wanafunzi na vituo vya afya katika jimbo la Misungwi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amehitimisha ziara yake ya
kikazi ya siku mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na Misungwi
mkoani Mwanza iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
pamoja na kuzungumza na watumishi wa umma kwa lengo la kutatua kero
na changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa halmashauri hizo.
Search for all messages with label Inbox