KIMATAIFA

SNAPCHAT WAINGIZA BILIONI 38 KWA MWEZI

SNAPCHAT WAINGIZA BILIONI 38 KWA MWEZI

Kampuni ya mtandao wa kijamii SNAP INC inayomiliki application ya SNAPCHAT wametoa taariifa na kusema idadi ya wanaotumia huduma ya kulipia kwenye mtandao huo inayoitwa SNAPCHAT PLUS imefikia Millioni 4 tangu ilipozinduliwa June mwaka jana.

Unaweza kujiuliza hii SnapchatPlus ni nini? sawa, ilivyo ni kama Snapchat ya kawaida lakini utofauti wake ni kwamba mtumiaji wake anapata uwezekano wa kupata maboresho ya ziada ndani ya Application hiyo ikiwemo filter na akili bandia ambayo kwa sasa inapatikana kwenye mtandao huo “My AI”

Unaweza kutamani kufahamu gharama za kulipia hii SnapChatPlus kwa mwezi, sawa jibu ni Dola 3.99 ambayo kwa pesa ya ki-Tanzania ni 9,634 kwa hesabu hiyo basi kwa watu milioni 4 ambao wamelipia huduma ya SNAPCHATPLUS inawafanya SnapChap kufanikiwa kukusanya pesa za ki-Tanzania Billioni 38,536,000,000

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *