Raisa Said,Tanga

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga imewataka wananchi kutimiza wajibu wao kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuomba wagombea au kuwa sehemu ya kutoa rushwa kwa wanachama.

Wito huo umetolewa na Frank Mapunda kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha robo mwaka April-June 2024.

” kwa kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa popote mwananchi ulipo timiza wajibu wako kwa kutojihusha na vitendo vya rushwa maana hata dini zetu zinakataza rushwa” alisisitiza Mapunda ambaye pia ni Ofisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga.

Mapunda alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara ya 8(1)[a] inatamka kuwa ” Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii” na ibarabya 8(1) [c] inatamka kuwa ” serikali itawajibika kwa wananchi”.

Katika utekelezaji vwa ibara hii ibara ya 5 imezungumza kwa kina juu ya haki ya kupiga kura inayompa kila mwananchi hakibna mamlaka ya kuamuabnani awe kiongozi na katika nafasi gani.” Hivyo ni rai yangu kwa wananchi kuwa waitumie haki yao kwa kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo bwasiotokana na rushwa.

Akiendelea kutoa taarifa alieleza kuwa katika kipindi hicho cha April -june 2024 kazi walizofanya ni uelimishaji kwa wajumbe wa kamati za afya ya msingi katika zahanatin, vituo vya afya na hospital pamoja na watumishibna wataalam wa sekta ya afya ambao ni 485 kwa idadi yao katika wilaya za kilindi , Handeni , korogwe na Lushoto.

Katika uelimishaji huo waliweka kipaumbele ushirikishaji wadau katika uzuiaji rushwa kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Halmashauri zote katika wilaya hizo.

Aidha katika utekelezaji jukumu la uzuiaji rushwa wamefanya chambuzi za mifumo sita ili kupata tija ya mfumo imara isiyokuwa na mianya ya rushwa na kukwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na utendaji kazi za serikali kwa ujumla.

Uchambuzi wa mifumo uliofanywa ni utoaji ufuatiliaji wa ushuru wa machinations ya share jijini Tanga, changiji huduma za usafiri kwa gari ya kubeba wagonjwa (ambulance) wagonjwa wanaopewa rufaa kutoka hospital ya wilaya ya pangani kwenda hospital rufaa mkoa wa Tanga bombo , ukusanyaji wa mapato na uchangiaji huduma za afya pangani pamoja na mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya machine za pos katika halmashauri za lushoto , bumbuli na pangani.

Wakati huo huo ameendelea na ufua utekelezaji wa miradi ya maendeleo 79 yenye thamani ya sh 34, 517, 081, 773.60 katika sekta za kipaumbele ambazo ni elimu , barabara , maji na afya

About Author

Bongo News

1 Comment

    Thanks for this post, I am a big fan of this internet site would like to go on updated.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *