KITAIFA

TANI 13 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA PAMOJA NA WATUMIA 4983

TANI 13 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA  PAMOJA NA WATUMIA 4983

Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya hapa Nchini limefanikiwa kukamata tani 13 .717 za dawa za kulevya Pamoja na watuhumiwa 4987 katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa kitengo cha kuzuia nakupambana na dawa za kulevya
Nchini kamishna msaidizi wa Polisi, ACP. Amon Kakwale amesema katika kipindi cha
kuanzia Januari hadi Juni 2023, ambapo kitengo hicho cha kuzua na kupambana
na dawa za kulevya kilifanikiwa kukamata kiasi cha Kilogramu 9,358.77 sawa na
Tani 9.36 za dawa za kulevya aina ya Bhangi.


Ameongeza kuwa tani 4.357 za Mirungi, kilogramu 1.86 za Heroin pamoja na
gramu 220.05 za Cocaine zilikamatwa na ekari 105.25 za mashamba ya bhangi na
mirungi yalitekeketezwa.
Katika hatua nyingine ACP Kakwale amesema Operesheni hiyo ilifanikiwa
kukamata watuhumiwa 4983 ambapo kesi 3784 zilifunguliwa ambapo kesi hizo
zipo katika hatua mbalimbali Mahakamani.
Mkuu huyo ametoa onyo kwa wanaoendelea kujihusisha na biashara haramu ya
dawa za kulevya kuacha mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa
kwa wakijihusisha na vitendo hivyo.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *