KITAIFA

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA YOGA DUNIANI

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA YOGA DUNIANI

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi
Yakubu akishiriki mazoezi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Yoga Duniani ambayo
huadhimishwa Juni 18, kila mwaka ambayo yamefanyika katika viwanja vya Gym Kana
jijini Dar es salaam.kwa Tanzania na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Balozi
wa India nchini Bw. Binaya Srikanta Pradhan na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Bw. Zlatan Milišić.

Tanzania imeadhimisha Siku ya Yoga Duniani huku Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikisisitiza kuunga mkono sherehe za kitamaduni za mataifa mbalimbali duniani kwa sababu zinasaidia kujenga jamii ya kimataifa kuwa wamoja.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Yoga Duniani ambayo huadhimishwa Juni 18, kila mwaka ambapo kwa Tanzania yamedhuiriwa na watu mbalimbali ambao wamefanya mazoezi ya Yoga kwa pamoja katika viwanja vya Gym Kana jijini Dar es salaam.

“Huu ni mwaka wa tisa sasa tangu Umoja wa Mataifa ulipotambua na kuupa mchezo wa Yoga siku maalum, Ubalozi wa India umeandaa sherehe hizi ambazo zimehuidhuriwa na watu zaidi ya 1000 kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo India na Tanzania” amesema Bw. Yakubu.

Mchezo wa Yoga asili yake ni India unaosaidia kuufanya mwili kuwa imara kwa kupata mazoezi kuanzia kichwani hadi miguuni hatua inayofanya mwili kuwa imara na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza. 

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kulia)
akiongea na Balozi wa India nchini Bw. Binaya Srikanta Pradhan wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Yoga Duniani yaliyofanyika Juni 18,2023 katika viwanja vya
Gym Kana jijini Dar es salaam.

Miongoni mwa washiriki wa maadhimisho hayo ni Balozi wa India nchini Bw. Binaya Srikanta Pradhan na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini nchini Bw. Zlatan Milišić ambapo kwa Tanzania Siku ya Yoga imeadhimishwa katika mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Arusha, Zanzibar na Kilimanjaro.

About Author

Bongo News

2 Comments

    https://kupit-kvartiruspb.ru в новостройках Санкт-Петербурга. Цены и фотографии квартир от застройщика в готовых и строящихся ЖК. Подбор жилья, ипотечные программы, сопровождение сделок и выгодные предложения.

    купить квартиру в Санкт-Петербурге в новостройке квартира в новостройке

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *