KITAIFA

TANZANIA YASISITIZA MIKAKATI HIFADHI YA BIONUAI MKUTANO WA GEF

TANZANIA YASISITIZA MIKAKATI HIFADHI YA BIONUAI MKUTANO WA GEF

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa pili kulia) akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika kushiriki Mkutano Mkuu wa Saba wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) unaofanyika Vancouver nchini Canada kuanzia tarehe 22 hadi 26 Agosti, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Hifadhi ya Bioanuai, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Thomas Bwana.

Tanzania imepokea na kupongeza azimio la kuanzishwa kwa Mfuko wa
Mazingira wa Dunia (GEF) na kusisitiza kuwezesha utekelezaji wa Mkakati wa
Dunia wa Kuhifadhi Bioanuai kupitia Mikakati ya Kitaifa ya Kuhifadhi Bionuai.
Hayo yamebainishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Saba wa Mfuko wa
Mazingira wa Dunia (GEF) unaofanyika Vancouver nchini Canada ambapo
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakati anaongoza
Ujumbe wa Tanzania kushiriki.
Pamoja na kuzipongeza nchi zilizotoa ahadi ya kuchangia Mfuko huo, Tanzania
imeziomba nchi zilizoendelea na zinazoendelea kuwezesha ukusanyaji wa
fedha za kutosha katika Mfuko husika.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Tanzania unaoshiriki Mkutano Mkuu wa Saba wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) Vancouver Canada ambao unafanyika kuanzia tarehe 22 Agosti, 2023 na kutarajiwa kuhitimishwa tarehe 26 Agosti, 2023


Mfuko wa Mazingira wa Dunia ni moja ya Mifuko wa Kimataifa inayowezesha
shughuli za uhifadhi wa mazingira duniani hususan katika nchi zinazoendelea.
Shughuli zinazowezeshwa ni pamoja na Hifadhi ya Bioanuai, Mabadiliko ya
Tabianchi, Matumizi bora ya Ardhi, Udhibiti wa Taka hatarishi na Kemikali
pamoja na Hifadhi ya maji yanayovuka mipaka.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofaidika na mfuko huu katika kuwezesha
shughuli za kuhifadhi mazingira nchini.
Pamoja na mambo mengine, moja ya masuala muhimu yaliyopitishwa na
Mkutano Mkuu wa GEF ni kuanzishwa kwa Mfuko wa Dunia Kuhifadhi
Bioanuai.
Watalaamu wengine kutoka Tanzania wanaoshiriki ni Mshauri wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa masuala ya Mazingira na Mabadiliko ya
Tabianchi, Dkt. Richard Muyungi, Mkurugenzi Msaidizi, Hifadhi ya Bioanuai
Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Thomas Bwana, Afisa
Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Thomas Chali na
Bw. Charles Faini wa Ubalozi wa Tanzania nchini Canada.
Mkutano huo umefunguliwa tarehe 22 Agosti 2023 unatarajiwa kuhitimishwa
tarehe 26 Agosti, 2023.

About Author

Bongo News

1 Comment

    Your article helped me a lot, is there any more related content? Thanks!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *