KITAIFA

TARURA WAZIDI KUZIFUNGUA BARABARA ZA VIJIJINI, SASA NI ZAMU YA IYEGEYA- LULANDA

TARURA WAZIDI KUZIFUNGUA BARABARA ZA VIJIJINI, SASA NI ZAMU YA IYEGEYA- LULANDA



MUFINDI: Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na ujenzi wa barabara ya Iyegeya- Lulanda yenye urefu wa Km 10.4 kwa kiwango cha lami kwa kutumia Teknolojia mbadala ya ECO Roads ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya Serikali ya kupunguza gharama za ujenzi na matengenezo ya barabara na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi na kusafirisha mazao yao kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa ziara maalum ya ukaguzi wa mradi huo, Meneja wa TARURA Mkoa wa Iringa Mhandisi Makori Kisare ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo uliofikia asilimia 50 ya utekelezaji na kubainisha kuwa matarajio makubwa ni kukamilika kwa mradi huo ndani ya muda uliopangwa.

“Kasi ya utekelezaji wa mradi huu ni kubwa na matarajio ni kwamba mradi huu utakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi ili waweze kusafiri na kusafirisha mazao yao kwa urahisi kutoka eneo la Sawala hadi Lulanda”, amesema Mhandisi Makori.

Barabara hiyo ya Iyegeya kwenda Lulanda tayari Mkandarasi anaendelea na hatua mbalimbali za utekelezaji na ujenzi wake unatarajia kukamilika ifikapo Agosti 2024.

Barabara ya Iyegeya- Lulanda inajengwa ikiwa ni mwendelezo wa barabara ya Sawala-Mkonge-Iyegeya kilomita 30 ambazo tayari zilishajengwa kupitia mradi wa Agri-Connect.

About Author

Bongo News

6 Comments

    priligy 30mg Abdominal radiography does not have the same level of sensitivity or specificity, but air fluid levels, signs of bowel dilation, and peritoneal calcifications can be used to suspect EPS in the setting of intestinal obstruction

    priligy dapoxetine 60mg To our knowledge, this is the first study to compare the combination of bolus and continuous infusion of hypertonic saline plus furosemide versus hypertonic saline alone in patient with TBI, and to compare sNGAL and sCr as marker for diagnostic and monitoring purposes

    Mishel, USA 2022 05 05 06 08 49 dapoxetine for premature

    Testosterone Undecanoate Application cost of cheap cytotec without rx In certain embodiments, R 8 is NH Cbz

    where can i get cheap cytotec pills I was taking it at night but I just started doing half in the morning and half at night

    Creatinine concentrations in blood and urinary samples were determined by routine procedures Hitachi Autoanalyser, Boehringer Mannheim what does lasix do I hope we get our BFPs soon

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *