Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya kilomita 13.8 ya Mji wa Mwanga wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua miradi ya miundombinu ya elimu na barabara Wilayani Mwanga.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Deogratius Ndejembi ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini
(TARURA) kwa kujenga barabara mpya yenye urefu wa kilomita 13.8
katika Mji wa Mwanga itakayowawezesha wananchi kufika eneo lililokuwa
halifikiki kwa urahisi.
Mhe. Ndejembi ametoa pongezi hizo akiwa Wilayani Mwanga wakati wa
ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu na
barabara inayotekelezwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia miradi ya
BOOST, SEQUIP, GPE LANES pamoja na TARURA.
Mhe. Ndejembi amesema TARURA imefanya na inaendelea kufanya kazi
kubwa katika ujenzi wa barabara hiyo na kuongeza kuwa, imetekeleza kwa
vitendo kaulimbiu yake isemayo ‘kukufungulia njia kufika kusiko fikika’
kwani itawawezesha wananchi wa Mwanga kufika eneo lililokuwa ni
changamoto kufikika.
Aidha, Mhe. Ndejembi amtaka Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya
ya Mwanga Mhandisi David Msechu kuhakikisha anasimamia vizuri
matumizi ya fedha za ujenzi wa barabara hiyo ili kusitokee mtu yeyote
atakeyekwamisha jitihada za Serikali za kuimarisha miundombinu hiyo.
“Tunataka ijengwe barabara yenye viwango ambayo itakayodumu kwa
muda mrefu ili iwe na tija kwa wananchi na maendeleo ya taifa na ndio
maana Serikali inahimiza matumizi ya teknolojia mpya ili barabara hiyo
ikikamilika idumu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Wilaya ya Mwanga Mhandisi
David Msechu amesema, gharama ya mradi huo kwa awamu ya kwanza ni
bilioni 4.99 ambazo zitawezesha ujenzi wa madaraja 16 na kufungua
kipande kilichokuwa hakipitiki.
Mhandisi Msechu amefafanua kuwa, lengo la mradi huo ni kuimarisha
miundombinu ya barabara ili kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwa
kuboresha sekta ya usafiri na usafirishaji na kuongeza kuwa, ukikamilika
utakuza mji wa mwanga, kupunguza msongamano wa magari pamoja na
kuwezesha huduma za kijamii zikiwemo za afya na elimu.
“Utekelezaji wa mradi huu ulianza Januari 04, 2023 na unatarajiwa
kukamilika Januari 04, 2024 kwa mujibu wa mkataba na mpaka sasa
mkandarasi amefikia asilimia 45 ya ujenzi na ameshalipwa milioni 829,”
Mhandisi Msechu amefafanua.
Naye, Mbunge wa Mwanga Mhe. Joseph Tadayo amesema ujenzi wa
mradi huo wa barabara ni wa kimkakati hivyo anatamani ukamilike kwa
wakati ili kuboresha huduma ya usafiri na usafirishaji kwani jirani na eneo
hilo pia kuna ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ambao ukikamilika
utaongeza uhitaji wa matumizi ya barabara hiyo.
1 Comment
Table 4 Association of therapeutic decision making by clinical and breast cancer characteristics, CYP2D6 phenotype, previous knowledge of CYP2D6 testing, referral method, and interest in CYP2D6 testing priligy buy online usa Benadryl is commonly used to treat itchiness in dogs caused by skin allergies, and it also reduces many of the other symptoms of allergies, including Hives