Leo tarehe 30 June 2024 Team ya watalamu kutoka EWURA imefika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kufuatilia na kufanya tathmini ya kina juu ya swala la bili za Maji.
Hii imetokana na malalamiko ya wananchi wa mji wa Maswa kwa Katibu Mwenezi Ndugu Paul Makonda kwa Mamlaka ya Maji ya Maswa kusadikika kutoza bili kubwa ya Maji.
Baada ya malalamiko haya yaliyotoleea jana tarehe 29 Jan,2023 Ndugu Paul Makonda aliwasiliana moja kwa moja na Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ambaye alitoa ahadi kwamba ndani ya siku moja angewaelekeza Mamlaka inayohusika na upangaji wa Bei ya Maji EWURA kufika na kufanya tathmini upya na kuja na ushauri juu ya kiwango sahihi cha wananchi kuchangia huduma ya Maji.