Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega, ameweka wazi mafanikio makubwa ya serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa miundombinu, akifichua kuwa kilometa 1,366 za barabara zenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 zimekamilika nchini, huku madaraja makubwa yakijengwa na kukamilika kwa kasi ya hali ya juu.

Akizungumza leo Februari 26, 2025, katika mkutano wa hadhara wilayani Pangani mkoani Tanga, ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Ulega amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha maendeleo yanafika kwa wananchi wote.

“Ulipoingia madarakani, ulikuta barabara na madaraja yakiendelea kujengwa. Kwa kauli yako ya Kazi Iendelee, madaraja manane yenye thamani ya shilingi bilioni 381 umeyakamilisha, yakiwemo Tanzanite, Kitengule, na Msingi pale Singida. Haya yote ni mapinduzi makubwa kwa Watanzania,” alisema Ulega.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo ameeleza kuwa miradi mikubwa ya barabara inaendelea kwa kasi, ikiwemo ujenzi wa kilometa 2,031 za barabara zenye thamani kubwa kwa taifa.

“Barabara ya Bagamoyo (Makurunge) – Mkange – Tungamaa – Pangani – Tanga inayoendelea kujengwa ni ushahidi wa dhamira yako thabiti Mheshimiwa Rais. Barabara hii itaunganisha mikoa na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Bagamoyo, Chalinze, Pangani na Tanga,” alieleza.

Waziri Ulega pia amezungumzia ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525, ambalo litakuwa na taa 240 za barabarani, huku mji wa Pangani ukipata taa 200 zaidi, kuhakikisha usalama wa wananchi na kuboresha mandhari ya eneo hilo.

“Kama haitoshi, umeweka msisitizo kwamba kila barabara inayojengwa iwe na taa za barabarani. Wizara ya Ujenzi imechukua agizo lako kwa uzito mkubwa, na tunahakikisha kila mradi unakamilika kwa viwango vya juu,” alisema.

Akitilia mkazo kasi ya ujenzi wa miradi hiyo, Waziri Ulega amesema kuwa wakandarasi wanahimizwa kufanya kazi bila kusita.

“Wakandarasi hawatudai sisi, bali sisi tunawadai kazi. Hapa hakuna kucheka, hakuna relax mpaka kazi ikamilike. Tutasimamia kila kitu usiku na mchana kwa maendeleo ya Watanzania,” alisisitiza Ulega.

About Author

Bongo News

4 Comments

    I like what you guys are up too. Such clever work and reporting! Keep up the excellent works guys I’ve incorporated you guys to my blogroll. I think it’ll improve the value of my website :).

    Mostbet umożliwia szybkie i bezpieczne transakcje finansowe. | Mostbet oferuje transmisje na żywo z wybranych wydarzeń sportowych. | Dołącz do turniejów i wyzwań organizowanych przez Mostbet. | Korzystaj z promocji cashback dostępnych w Mostbet. mostbet opinie

    I gotta favorite this web site it seems very beneficial very beneficial

    1win platformasında qeydiyyat prosesi çox sadə və sürətlidir | 1win platformasında yeni başlayanlar üçün təlimatlar mövcuddur | 1win-də müxtəlif idman növlərinə mərc etmək imkanı var | 1win mobil tətbiqi ilə oyun təcrübəsini artırın​1win platformasında istifadəçilər üçün müxtəlif bonuslar təqdim olunur | 1win platformasında istifadəçilər üçün müxtəlif kampaniyalar mövcuddur​1win mobil tətbiqi ilə istənilən yerdə oyun oynayın | 1win az saytında müxtəlif ödəniş üsulları mövcuddur | 1win azərbaycan saytında istifadəçilər üçün müxtəlif təlimatlar mövcuddur | 1win az saytında istifadəçilər üçün rahat interfeys mövcuddur | 1win-də müxtəlif ödəniş üsulları ilə rahatlıqla pul yatırın​ 1win promo kodu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *